Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA

Mapigano makali yarindima kati ya makundi hasimu ya wanajihadi kaskazini mwa Mali

Kaskazini mwa Mali, mapigano makali yameendelea kati ya makundi mawili hasimu ya wanajihadi katika ukanda wa Sahel tangu mwanzoni mwa mwezi huu. Kwa upande mmoja, kundi la Jnim (kundi linalodai kutetea Uislamu na Waislamu), lenye mafungamano na al-Qaedana kwa upande mwingine, EIGS, tawi la kundi la Islamic State nchini Mali.

Wapiganaji wa kijihadi nchini Mali.
Wapiganaji wa kijihadi nchini Mali. © AP / STR
Matangazo ya kibiashara

Mapigano hayo yanapamba moto katika eneo linalojulikana kama "mipaka mitatu" (Mali-Burkina-Niger) na hasa katika mkoa wa Gao, karibu na mji wa Tessit. Mwanzoni, ilikuwa ni kundi la Jnim lililodhibiti eneo hilo, kutokana na idadi kubwa ya wapiganaji wake kutoka katikati mwa Mali na Burkina Faso.

Lakini tangu Jumatatu, wapiganaji wa EIGS, wengi wao wakiwa nchini Niger na Burkina, wamekuwa wakirejea kwa nguvu katika eneo la Tessit, ambalo walikuwa wamelidhibiti kwa miezi kadhaa. Mapigano hayo, ambayo tayari yamesababisha vifo katika pande zote mbili, lakini pia kati ya raia, yanaendelea.

Vyanzo vingi vya usalama nchini Mali na kimataifa, wenyeji wa maeneo haya na mashirika ya kiraia wanathibitisha kwamba wenyeji wa vijiji kadhaa kama vile Tadjalalt, Tinagghy, Bakal au hata Kaygoutan walilazimika kutoroka makazi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.