Pata taarifa kuu
UGANDA-HAKI

Uganda yadai ICJ 'haikuitenda haki’ kufuatia uamuzi wake katika mzozo na DRC

Baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki siku ya Jumatano kuiamuru Kampala kulipa dola milioni 325 za fidia kwa jirani yake kwa kuhusika katika uharibifu uliosababishwa wakati wa vita vya pili vya Kongo kati ya mwaka 1998 na 2003, Uganda inaona kuwa haijatendewa haki.  

Mahakama ya Kimataifa ya Haki huko The Hague.
Mahakama ya Kimataifa ya Haki huko The Hague. AP - Peter Dejong
Matangazo ya kibiashara

Ni uamuzi "usio wa haki na mbaya" kwa mujibu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uganda. Katika taarifa, mamlaka inasema DRC imeshindwa kutoa ushahidi wa kina wa madhara yaliyosababishwa na majeshi ya Uganda wakati wa vita vya pili vya Kongo.

Wizara pia inasikitishwa na uamuzi unaokuja wakati "nchi hizo mbili zikiimarisha uhusiano wao", na kufanya kazi pamoja katika nyanja za usalama, miundombinu na ushirikiano wa kiuchumi wa kikanda.

Kampala inadai kujadiliana na Kinshasa ili kupata suluhu la kudumu na linalokubalika la mzozo huo, bila kubainisha iwapo serikali italipa fidia iliyo sawa na dola milioni 325.

Awali Rwanda ilihusishwa katika mzozo

Katika kesi hiyo, Kinshasa pia ilikuwa imewasilisha mashtaka kwa ICJ dhidi ya Rwanda mshirika mwingine wa vita hivyo, lakini ombi hilo halikufaulu.

Baada ya kuwasilsha kwa mara ya kwanza mashtaka dhidi ya Rwanda mwaka 1999 katika mahakama ya kimataifa, mashtaka ambayo hata hivyo hayakutiliwa maanani, serikali ya Kinshasa iliwasilisha kwa mara nyingine tena mashtaka mwaka 2002 ikiituhumu Rwana kuivamia Congo Agost mwaka 1998 ambapo kulitokea mauaji na uvunjifu wa haki za binadamu lakini pia uporaji wa rasilimali za Congo. 

DRC ikaiomba Mahakama kuamuru Rwanda kuviondoa vikosi vyake nchini Congo na kuitaka ilipe fidia kutoka na uharibifu ambao  hata hivyo haikutaja kiwango. Mahakama hiyo ilishindwa kusikiliza kesi hiyo baada ya Rwanda kutangaza kutokuwa na imani na mahakama hiyo. Februari 2006 Mahakama hiyo iliatangaza kutokuwa na uwezo wa kusikiliza kesi ambayo iliwasilisha na Congo mwaka 1999 ikiyatuhumu mataifa ya Rwanda, Burundi na Uganda katika vita vya pili vya uvamizi wa Congo. 

Ni kesi pekee kuhusu Uganda ndio iliosikilizwa hadi mwisho na mahakama hiyo ya kimataifa ya Haki. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.