Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

Serikali ya DRC yathibitisha njama za kutaka kuhatarisha usalama wa taifa

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,uchunguzi umebaini kuwa, kuna ushahidi kuonesha nia ya kutikisa utawala wa rais Felix Tshisekedi.

Moja ya maeneo ya mji mkuu wa DRC, Kinshasa.
Moja ya maeneo ya mji mkuu wa DRC, Kinshasa. John Wessels/Bloomberg via Getty
Matangazo ya kibiashara

Taarifa iliyosomwa kwenye Televisheni ya taifa na msemaji wa rais, Kasongo Mwema imeeleza kuwa kuna njama za kutikisa taasisi za kidemokrasia nchini humo, ambazo amesema haziwezi kukubaliwa.

Hii imekuja baada ya kukamatwa kwa François Beya, mshauri wa masuala ya usalama wa rais Tshisekedi Jumamosi iliyopita kwa madai ya kuwa na njama za kudhoofisha usalama wa taifa, wakati rais wa nchi hiyo alipokuwa anahudhuria mkutano wa viongozi wa Afrika jijini Addis Ababa.

Kukamatwa kwa Beya, kulizua maandamano jijini Kinshasa, huku kukiwa na hofu na hata madai ya kuwepo kwa mipango ya kumpindua rais Thisekedi.

Serikali inasema hali ni tulivu lakini uchungizi wa kina unaendelea, lakini haijaeleza kwa wazi ni uchunguzi wa aina gani unaoendelea dhidi ya Beya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.