Pata taarifa kuu

Vladimir Putin athibitisha kuwepo kwa mamluki wa Urusi nchini Mali

Nchini Mali, kumekuwa na utata kwa miezi kadhaa kuhusu kuwepo kwa kampuni ya usalama ya kibinafsi la Wagner kutoka Urusi. Siku ya Jumatatu, Rais wa Urusi Vladimir Putin mwenyewe ambaye alizungumza tofauti na mamlaka ya mpito nchini Mali kwa kukanusha uhusiano wowote kati ya mamluki kutoka kampuni hio na serikali ya Urusi.

Rais Vladimir Putin wakati wa mkutano na waandishi wa habari kufuatia mkutano wake na Emmanuel Macron, Februari 7, 2022.
Rais Vladimir Putin wakati wa mkutano na waandishi wa habari kufuatia mkutano wake na Emmanuel Macron, Februari 7, 2022. REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Kwa wiki kadhaa, nchi kumi na tano za Ulaya, ikiwa ni pamoja na Ufaransa, lakini pia Canada au, hivi karibuni zaidi, Marekani, wamedai kuwa mamluki mia kadhaa wa Kirusi wanatumwa nchini Mali.

Madai ambayo yameendelea kukanushwa kabisa na mamlaka ya mpito nchini Mali, ambayo inadai kuwa hii ni kampeni ya kuichafua Mali na kwamba wapiganaji wa Urusi wanaounga mkono vikosi vya Mali sio mamluki bali ni wanajeshi, waliopo nchini Mali kwa msingi wa ushirikiano kati ya Mali na Urusi.

"Nchi ya Urusi haina uhusiano wowote na kampuni hizi zinazofanya kazi nchini Mali"

Lakini siku ya Jumatatu, Rais wa Urusi Vladimir Putin alipinga hotuba ya mamlaka nchini Mali kwa kukataa uhusiano wowote kati ya mamluki hao na serikali ya Urusi. "Kuhusu Mali, Rais (Emmanuel Macron) alizungumzia suala hili mara kadhaa, tumelijadili na Rais anajua msimamo wetu: serikali ya Urusi, taifa la Urusi halina uhusiano wowote na kampuni hizi ambazo zinazofanya kazi nchini Mali," Rais wa Urusi amesema wakati wa mkutano na waandishi wa habari na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron.

"Tunachojua, hakuna maoni yoyote ambayo yametolewa na viongozi wa Mali kuhusiana na shughuli za kibiashara za kampuni hizi," ameongeza wakati alipoulizwa na mwandishi wa habari. "Kulingana na mantiki ya jumla ambayo inatumika kwa NATO, wanachama wa Muungano na wanachama wa baadaye wa Muungano, ikiwa Mali itachagua kufanya kazi na kampuni zetu, ina haki ya kufanya hivyo. Lakini nataka kusisitiza kwamba serikali ya Urusi haina uhusiano wowote na hili. Kuna masilahi ya kibiashara ya kampuni zetu, wanajadiliana na viongozi wa nchi hiyo, "amehitimisha rais wa Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.