Pata taarifa kuu
Africa - Ukeketaji

Dunia yaungana kuadhimisha siku ya kimataifa ya kupinga ukeketaji

Tarehe sita mwezi Februari, dunia iliungana kuadhimisha, Siku ya kimataifa ya kupinga vitendo vya ukeketaji kwa wasichana na wanawake, ambapo nchini Kenya wanaharakati wameamua kuwatumia vijana wa kiume na michezo kufanya kampeni kumaliza vitendo hivyo.Carol Korir ,amezuru eneo la Kajiado nchini Kenya na kutuandalia  ripoti ifuatayo.

Vijana wakicheza mpira
Vijana wakicheza mpira © rfi
Matangazo ya kibiashara

Kwa muda sasa, mapambano dhidi ya ukekekataji, yameongozwa na wanaharakati wa kike, lakini Kuvishinda vita hivyo wameamua kubadili mbinu.

Katika eneo la Maili Tisa ,eneo jirani na Bisil,Kajiado,sauti za wavulana wa Kimaasai marufu Moran,wanatembea kwa pamoja kuelekea kwenye uwanja wa kuchezea mpira wa miguu.

Hawa ni wanaume ambao wamejumuishwa katika mapambano dhidi ya ukeketaji, na ni kwa kuwa wanaousemi mkubwa kwenye jamii yao.

« Tunasema utamu wa ndoa ubaki ;Tunaweza kuoa wanawake ambao hawajakeketwa, » wanaimba wakingia kwenye uwanja wa michezo.

Kupitia michezo, wanaungana na wenzao kwa lengo la kuwahimiza kuachana na mila hii potofu dhidi ya wanawake, hwa ni baadhi ya niliozungumza nao katika eneo la Bisil, Kajiado

« Tumekuja kucheza mpira kwa pamoja na tukumbushane ,ukielekea nyumbani,elezea wazazi,tukatae FGM , »alisema mmoja.

« Tuoe kama kawaida na tuache mambo ya ukeketaji, » alisema mchezaji wa pili.

Agnes Leina, mkurugenzi wa shirika la Ilara Matak Community Concerns, ni miongoni mwa mashirika yanayoratibu kampeni hii.

«  Hao champions ni wale sasa wataenda kuelekeza na kusema sisi tuko tayari kuwaoa wasichana ambao hawajakeketwa na tuko tayari  kuwalinda wasichana ambao ni dada zao.

« Eneo lingine Kenya,msichana wa miaka 14 yuko shule,yuko sekondari, lakini hapa kwetu,yuko nyumbani ameolewa,kwa hiyo inakuwa ni  hali ya umaskini inajirudia, »alisema Agnes Leina.

Roy Sesaka Telewa, afisa mkuu mtendaji wa baraza la vijana nchini Kenya ,anasema michezo ni lugha sahihi ya kuwafanya jinsia ya kiume kukumbatia ujumbe wa kumalizwa ukeketaji.

 

« Vijana ndio watamaliza ukeketaji,na tunatumia njia bunifu ,ya michezo kufikisha ujumbe huo, »alisema Roy Sesaka Telewa.

Bodi ya kupambana na ukeketaji nchini Kenya inasema vitendo vya ukeketaji nchini Kenya kwa sasa imeshuka hadi kufikia asilimia 21 isipokuwa katika maeneo wanayokaa jamii ya wafugaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.