Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

DRC: Watu zaidi ya 20 wauawa katika shambulio katika kambi ya wakimbizi Ituri

Nchini DRC, kumetokea mauaji mengine usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano wiki huko Djugu, katika mkoa wa Ituri, kaskazini mashariki mwa nchi.

Gari la kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini DRC likishika doria Machi 13, 2020 kuelekea Djugu, huko Ituri.
Gari la kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini DRC likishika doria Machi 13, 2020 kuelekea Djugu, huko Ituri. © Samir Tounsi / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na Jeshi, zaidi ya watu 20 wameuawa katika shambulio katika eneo la watu waliotorokamakazi yao. Kulingana na vyanzo kutoka eneo hilo, idadi ya watu waliouawa ni kubwa. Kitengo cha usalama katika ukanda wa Kivu, mradi unaoongozwa na shirika la kimataifa la kutetea Haki za Binadamu la Human Rights Watch limesema kuwa zaidi ya watu 40 wameuawa. Jeshi, kwa upande wake, limebaini kwamba zaidi ya watu 20 ndio wameuawa katika shambulio hilo.

Washambuliaji waliwasili katika eneo hilo takriban kilomita kumi na mbili kutoka katikati mwa mji wa Djugu, saa tatu usiku kwa saa za huko. Waliwafyatulia risasi watu hawa waliotoroka makazi yao kwa kuhofia usalama wao. Baadhi ya waathiriwa waliuawa kwa mapanga, kulingana na watu walionusurika. Wazee, watoto, walemavu ni miongoni mwa waliouawa.

Walinada amani wa Umoja wa Mataifa wanaopiga kambi kilomita kumi kutoka eneo la tukio, walifika nusu saa baada ya shambulio hilo. Baada ya kurushiana risasi kwa takriban saa mbili, walifanikiwa kuwafukuza wanamgambo hao na kulinda eneo hilo kwa muda wote wa usiku.

Ripoti ya mwisho itajulikana baadaye leo. Uchunguzi unaendelea. Baadhi ya waliokimbia makazi yao waliondoka eneo hilo na kukimbilia msituni. Miongoni mwao ni watu kadhaa waliojeruhiwa. Mashambulizi kwenye makambi ya wakimbi wa ndani yameongezeka katika miezi ya hivi karibuni huko Ituri, na hivyo kuzidisha mzozo wa usalama na kibinadamu katika eneo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.