Pata taarifa kuu
LIBYA-SIASA

Libya: Seif al-Islam atoa wito wa kuandaliwa kwa uchaguzi wa wabunge

Saif al-Islam Gaddafi avunja ukimya wake kwa mara ya kwanza baada ya kuahirishwa kwa uchaguzi uliopangwa kufanyika tarehe 24 Desemba.

Seif al-Islam Kadhafi, mtoto wa pili wa dikteta aliyeuawa Muammar Gaddafi, ndiye anayeshindaniwa zaidi kati ya safu ya wagombea wenye utata ambao wamejiandikisha kwa uchaguzi wa rais wa Libya.
Seif al-Islam Kadhafi, mtoto wa pili wa dikteta aliyeuawa Muammar Gaddafi, ndiye anayeshindaniwa zaidi kati ya safu ya wagombea wenye utata ambao wamejiandikisha kwa uchaguzi wa rais wa Libya. STRINGER libyan High National Electoral Comission FB Page/AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Mtoto wa dikteta wa zamani, Muammar Gaddafi, akiwahutubia Walibya katika taarifa ya Januari 27, alitangaza mpango wa kutatua hali iliyozuiwa tangu kushindwa kufanyika kwa uchaguzi wa urais na wa wabunge. Seif al-Islam anatoa wito wa kufanyika, kwanza na bila kuchelewa, kwa uchaguzi wa wabunge.

Nchi ya Libya iko katika hali ya mkanganyiko, hakuna tarehe ya uchaguzi ambayo, kwa kweli, imetangazwa. Nchi hiyo inaelekea kujiuzulu kwa serikali ya Dbeibah. Huu ndio wakati uliochaguliwa na Seif al-Islam kuzindua pendekezo lake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.