Pata taarifa kuu
LIBYA-UFISADI

Libya: Waziri wa tatu wa serikali akamatwa kwa rushwa katika kipindi cha mwezi mmoja

Uamuzi huo ulichukuliwa kama sehemu ya uchunguzi wa tuhuma za ufisadi wa kifedha na kiutawala dhidi ya Ali Zenati, Waziri wa Afya wa Libya.

Shutuma za ufisadi zinazowalenga wajumbe wa serikali ya umoja wa kitaifa hakika hazisaidii masuala ya Abdelhamid Dbeibah.
Shutuma za ufisadi zinazowalenga wajumbe wa serikali ya umoja wa kitaifa hakika hazisaidii masuala ya Abdelhamid Dbeibah. AP - Hazem Ahmed
Matangazo ya kibiashara

Kielezo cha mitizamo ya Ufisadi cha shirika la kimataifa la kupambana na ufisadi Transparency International, kilichotolewa wiki hii, kinaiweka Libya chini kabisa ya kiwango hicho. Imeorodheshwa ya 172 katika kiwango cha nchi 180, katika kiwango sawa na Equatorial Guinea. Ripoti hii ya kimataifa inafichuliwa wakati ambapo Mwanasheria Mkuu wa Tripoli aliamuru kumweka kizuizini Ali Zenati, Waziri wa Afya wa Libya na naibu wake wa pili, kwa tuhuma za ufisadi.

Mawaziri wa Elimu na Utamaduni wako chini ya vyombo vya sheria

Zenati ni waziri wa tatu katika serikali ya Dbeibah kuchunguzwa kwa ufisadi katika kipindi cha siku 35.

Tayari Desemba 20, Waziri wa Elimu aliwekwa kizuizini ikiwa ni sehemu ya uchunguzi wa upungufu wa jumla wa vitabu nchini. Mwishoni mwa mwezi Desemba, Waziri wa Utamaduni ndiye alikuwa ametoka tu kuwekwa kizuizini kama sehemu ya uchunguzi mwingine wa rushwa na ubadhirifu wa fedha za umma.

Kuzuiliwa kabla ya kesi kwa Waziri wa Afya na Naibu Waziri wake kunatokana, kulingana na Mwanasheria Mkuu wa Tripoli, juu ya "ushahidi wa kutosha wa wajibu wao kwa ukweli ambao wanashtakiwa".

Uuzaji wa vitengo vya uzalishaji wa oksijeni

Kulingana na chanzo hicho, Waziri wa Afya na naibu wake wa pili waliuza vitengo vya uzalishaji wa oksijeni, na kwa hadi 1000% ya bei ya ununuzi. Pia wametia saini mikataba moja kwa moja na kampuni zilizoanzishwa mnamo mwaka 2021 ambazo hazikidhi vigezo.

Kwa upande mmoja Waziri Mkuu wa Libya anakabiliwa kwa ipande mmoja na Bunge lenye shauku ya kuwekwa kwa serikali mpya, kwa upande mwingine maandamano ya watu wenye hasira kwa sababu ya kuzorota kwa uchumi na hali ya kijamii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.