Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-SIASA

Burkina Faso: Viongozi wa mapinduzi wakutana na mawaziri wa zamani katika ofisi ya rais

Nchini Burkina Faso, viongozi wa mapinduzi wanaendelea kujaribu kutuliza hali siku chache baada ya mapinduzi ambayo jumuiya ya kimataifa inaendelea kulaani. Siku ya Jumatano viongozi wa mapinduzi walikutana na mawaziri wa serikali ya zamani ya Roch Marc Christian Kaboré.

Ikulu ya Kossyam, makazi ya rais wa Burkina Faso, huko Ouagadougou.
Ikulu ya Kossyam, makazi ya rais wa Burkina Faso, huko Ouagadougou. Wikimedia Commons/ CC-BY-SA 3.0/Sputniktilt
Matangazo ya kibiashara

Kinyume na ilivyotangazwa na baadhi ya vyombo vya habari, mkutano ulifanyika katika ikulu ya rais, na si katika kambi ya jeshi ya Baba-Sy.

Mkutano huo ulifanyika katika hali ya utulivu kulingana na mmoja wa washiriki na uliongozwa na Luteni-Kanali Paul-Henri Sandaogo Damiba. Alishiriki mkutano huo Jenerali Aimé Barthelemy Simporé, Waziri wa zamani wa Jeshi. Waziri Mkuu Lassina Zerbo hakushiriki mkutano huo. "Ilikuwa ni mkutano wa kuwahakikishia," chanzo chetu kimeasema.

Usafiri wowote nje ya Ouagadougou hauruhusiwi

Mkuu wa utawala wa kijeshi amepiga marufuku mawaziri wa zamani ikiwa ni pamoja na maafisa wa zamani wa serikali kusafiri nje ya mji wa Ouagadougou, huku akibainisha kuwa hana nia mbaya dhidi yao. "Walihakikisha kwamba lengo lao sio kuwafanyia vitisho watu," ame waziri wa zamani, ambaye pia alishiriki katika mkutano huo.

Wawakilishi wa utawala wa kijeshi, mbali na hayo, wamewataka mawaziri wa zamani kutozuia hatua yao. "Wanasema wanahitaji kila mtu kufanya kazi," chanzo chetu kinmesema. Lakini hakuna ratiba ya kukutana na wanasiasa mbalimbali ambayo imetolewa hadi sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.