Pata taarifa kuu
SUDAN-SIASA

Sudan: Mahakama ya Sudan na Marekani walaani ukandamizaji dhidi ya maandamano

Uongozi wa Mahakama nchini Sudan umelaani hatua ya maafisa wa usalama kuendelea kuwashambulia waandamanaji wanaoendelea kushinikiza jeshi kuacha madaraka, huku Marekani ikisema inafikiria kuwachukulia hatua wale wanaokwamisha suluhu ya mzozo wa kisiasa nchini humo.

Waandamanaji kusini mwa Khartoum baada ya mapinduzi, Jumatatu Oktoba 25, 2021.
Waandamanaji kusini mwa Khartoum baada ya mapinduzi, Jumatatu Oktoba 25, 2021. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Kauli hii ya viongozi wa Mahakama imekuja wakati maandamano yakiendelea nchini humo na tangu jeshi ilipochukua madaraka mwezi Oktoba mwaka uliopita, watu zaidi ya 70 wamepoteza maisha kwa kupigwa risasi na maafisa wa usalama.

Wiki hii pekee, waandamanaji saba waliuawa jijini Khartoum siku ya Jumatatu na siku ya Alhamisi, maelfu ya waandamani walijitokeza kulaani mauaji hayo na kuushinikiza uongozi wa jeshi kuachia madaraka.

Naye mjumbe mpya wa Marekani kwenye pembe ya Afrika, David Satterfield ambaye amezuru nchi hiyo, amelaani maafisa wa usalama kuendelea kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji na kusisitiza kuwa Marekani, itawachukulia hatua wanaokwamisha mchakato wa demokrasia nchini humo.

Katika hatua nyingine, kiongozi wa kijeshi Jenerali Abdel Fattah al-Burhan amewateua Mawaziri 15, lakini hakumtaja Waziri Mkuu, Waziri wa Ulinzi na Usalama wa ndani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.