Pata taarifa kuu

Burkina Faso: Shule zaidi ya 3,000 zafungwa kwa sababu ya usalama

Takwimu hii ya kutisha ilitangazwa Jumatano, Januari 5, 2022, na msemaji wa serikali, Alkassoum Maïga, mwishoni mwa kikao cha Baraza la Mawaziri. Hii ni zaidi ya 13% ya shule za nchi.

Darasa likiwa halina wanafunzi na waalimu huko Burkina Faso.
Darasa likiwa halina wanafunzi na waalimu huko Burkina Faso. OLYMPIA DE MAISMONT / AFP
Matangazo ya kibiashara

Takwimu hii imekuwa ikiongezeka kwa miaka kadhaa. "Ni ya kushangaza sana na kuna sababu za wasiwasi," alisema msemaji wa serikali mwenyewe. Katika miaka mitatu, shule nyingine 1,300 zililazimika kusitisha shughuli kutokana na shinikizo la magaidi. Hali inayohusisha wanafunzi zaidi ya 500,000 na walimu karibu 15,000.

 

Serikali yafanya jitihada, inahakikisha hilo

Hata hivyo serikali inahakikisha, inafanya jitihada. Shule zaidi ya 200 zimefunguliwa hivi karibuni, 25 zimehamishwa katika maeneo yaliyoonekana kuwa salama. Kwa mujibu wa Alkassoum Maiga, wanafunzi zaidi ya 13,500 waliohamishwa ndani ya nchi waliweza kujiandikisha tena.

"Jitihada za serikali hazina maana, amesema Wendyam Zongo Wendyam, katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi katika Utawala na Usimamizi wa elimu na Utafiti. Hakuna maana yoyote ya kufunguliwa kwa shule, ikiwa watu waliolazimika kuyahama makaazi yao hawawezi kwenda nyumbani na kwa hiyo inatakiwa kwanza kurudi kwa usalama"

"Kurejesha usalama katika maeneo yaliyoathirika"

Ijumaa jioni, wakati wa hotuba yake kwa taifa akiukaribisha mwaka wa 2022, Rais Roch Marc Christian Kaboré, ameweka lengo kwa serikali mpya "kurejesha usalama katika maeneo yaliyoathiriwa na magaidi na wakimbizi wa ndani kurudi kwa makazi yao katika maeneo yao alikotoka".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.