Pata taarifa kuu
EU-AU-USHIRIKIANO

Mkutano kati ya Umoja wa Ulaya na Umoja wa Afrika kufanyika Februari 17 na 18

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwa sasa ndiye mwenyekiti wa Baraza la Umoja wa Ulaya tangu Januari 1 na Brussels itakuwa na sehemu kubwa ya diplomasia kati ya Ulaya na Afrika wakati wa mkutano wa kilele wa taasisi hizi mbili za kikanda Februari 17 na 18, 2022.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, baada ya mkutano wa kilele waUmoja wa Ulaya, EU, huko Brussels, Desemba 17, 2021.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, baada ya mkutano wa kilele waUmoja wa Ulaya, EU, huko Brussels, Desemba 17, 2021. AP - John Thys
Matangazo ya kibiashara

Baada ya ule wa Abidjan mwaka 2017, mkutano huu wa sita kati ya taasisi hizo mbili, ulioahirishwa hadi mwezi Oktoba mwaka uliyopita kutokana na janga la Covid-19, utafanyika, na watashiriki viongozi kutoka mabara haya mawili ambayo hayakubaliani juu ya mafaili yote ambayo yatawekwa mezani.

Emmanuel Macron atakuwa na mshirika wake mkubwa kabla na wakati wa mkutano huu: Macky Sall, ambaye atachukua uongozi wa Umoja wa Afrika mwanzoni mwa mwaka wa 2022. Wakuu hao wawili wa nchi, ambao pia walikutana kwa mazungumzo Desemba 20, wanaungana mkono.

Hata hivyo, kuahirishwa kwa mkutano huo hadi Septemba mwaka jana kulizipanga nchi 27 za Umoja wa Ulaya na nchi 55 wanachama wa Umoja wa Afrika, kwani kulikuwa na mambo mengi ya kutokubaliana juu ya mada zinazopaswa kujadiliwa. Na rais wa Senegal alitangaza hilo: wakati wa muhula wake kama mwenyekiti wa Umoja wa Afrika kutakuwa na ombi la kutaka malipo ya haki kwa maliasili na mabadiliko katika utawala wa kimataifa.

Covid yatia wasiwasi mabara yote mawili

Huko Brussels, nchi 27 wanachama wa Umoja wa Ulaya zinataka maendeleo katika "majibu dhidi ya janga la Covid-19"; juhudi za kusaidia bara la Afrika, kwa sasa, zimepunguzwa, kufungwa kwa mipaka mara tu kunapozuka kirusi kipya katika bara hilo. Umoja wa Ulaya, ambao tayari unapinga dhidi ya uwepo wa kampuni ya Wagner, kutoka Urusi inayotumia mamluki, bila shaka utajaribu kuweka uongozi wake - na kwa hiyo ule wa Ufaransa - katika masuala ya usalama.

Suala lingine, nyeti kila wakati, ambalo linaweza kusababisha mvutano: suala la kuhama. Kwa sababu janga hilo huongeza tu shinikizo la kiuchumi kwa mataifa ya Afrika, na hivyo kusababisha hali kuzorota zaidi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.