Pata taarifa kuu

Wanafunzi Burundi warejea shuleni, sasa kupimwa Covid 19

Msikilizaji tofauti na habari yetu tuliyoripoti mwishoni mwa juma lililopita, shule zimefunguliwa tena nchini Burundi baada ya likizo ya kawaida, zikifunguliwa huku maambukizi ya Covid 19 yakiendelea kuripotiwa ambapo mamlaka za afya sasa zikitaka wanafunzi na walimu kupimwa virusi hivyo.

Picha ikimuonesha raia wa Burundi akipimwa Covid 19, hapa ilikuwa ni Juni 6, 2020
Picha ikimuonesha raia wa Burundi akipimwa Covid 19, hapa ilikuwa ni Juni 6, 2020 AP - Berthier Mugiraneza
Matangazo ya kibiashara

Shule nchini humo zimefunguliwa hivi leo baada ya karibu miezi mitatu kuwa zimefungwa kwa mapumziko, ambapo sasa wanafunzi watakuwa wakipimwa ikiwa wana maambukizi ya virusi hivyo au la.

Katika mahojiano na gazeti la The East African, msemaji wa wizara ya afya nchini Burundi, Jean Bosco Girukwishaka, amesema itakuwa ni lazima kwa wanafunzi wa shule za msingi na Sekondari kufanya vipimo vya haraka vya Covid 19.

Wizara ya afya imesema zoezi la upimaji lilianza tangu Ijumaa ya wiki iliyopita kwa walimu na wanafunzi wa bweni ambapo linatarajiwa kumalizika Jumanne ya wiki hii.

Haya yanajiri wakati huu wizara ya afya nchini humo ikisema katika juma la Kwanza la mwezi September, maambukizi ya Covid 19 yameongezeka hasa katika jiji la Bujumbura na miji mingine, chanzo kikiwa ni raia kutofuata vema masharti ya kujikinga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.