Pata taarifa kuu
DRC-UGANDA

DRC-Uganda: Maelezo ya kwanza baada ya vifo 41 kufuatia ajali kwa boti

Idadi ya watu waliopoteza maisha katika ajali ya boti iliyozama kwenye Ziwa Albert, linalopatikana kwenye mpaka kati ya DRC na Uganda imeongezeka na kufikia 41.

Ziwa Albert kati ya Uganda na DRC
Ziwa Albert kati ya Uganda na DRC FILE PHOTO
Matangazo ya kibiashara

Miili 41 imeondolewa katika Ziwa Albert baada ya kuzama Jumatano, Desemba 23.

Boti hilo lililokuwa likitokea katika mkoa wa Ituri, mkoa wa DRC unaopatikana kwenye mpaka na Uganda kuelekea katika soko la Panyamur, nchini Uganda, lilizama usiku wa Jumatano baada ya kutokea kwa dhoruba kali.

Usiku huo, eneo la kuchimba la mtu wa Uganda, lililokuwa na abiria na vifurushi vya samaki wenye chumvi, lilielekea kwenye soko la Panyamur, lililoko nchini Uganda.

Ajali hiyo ilitokea karibu na kambi ya wavuvi ya Kolokoto, baada ya dhoruba kutokea amesema gavana wa Ituri, Jean Bamanisa.

Raia wa DRC na Uganda ni miongoni mwa watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo mbaya amesema kiongozi wa kijadi wa jamii ya Wangongo, huko Mahagi-Port. Miili ya wahanga hao tayari imerejeshwa kwa familia zao, ameongeza kiongozi huyo.

Kulingana na gavana wa mkoa wa Ituri, bado kuna idadi ya watu isiyojulikana ambao kufiki sasa wamekosekana. Zoezi la kutafuta miili ya watu hao linaendelea.

Kuhusu sababu za ajali hiyo hiyo, mamlaka katika mkoa wa Ituri imebaini kwamba boti hiyo ilikuwa imebeba mzigo kupita kiasi, upepo mkali na haswa ukweli kwamba boti hilo lilikuwa ikisafiri usiku.

Ajali kama hizi hutokea mara nyingi kwenye Ziwa Albert. Mnamo mwezi Juni, boti mbili zilizama, na kusababisha vifo vya watu 18.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.