Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-BREXIT

Brexit: Abidjan yatia saini mkataba wa biashara huria na London

Abidjan imetangaza wiki hii kwamba imehitimisha mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na London.

Alassane Ouattara, rais wa  Côte d'Ivoire.
Alassane Ouattara, rais wa Côte d'Ivoire. SIA KAMBOU/AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakati Uingereza ikijiondoa katika Umoja wa Ulaya, mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi hautatumika tena kwa soko la Uingereza kuanzia Januari 1, 2020.

Kwa upande wa Côte d'Ivoire, inasema London ni mshirika muhimu. Nchi nyingi za Afrika ziko katika hali hiyo na zimesaini mikataba na Uingereza.

Ikiwa Uingereza iko mbali kuwa soko muhimu kwa bidhaa kutoka Côte d'Ivoire, kwa upande mwingine, ni mshirika wa kimkakati katika suala la kifedha.

Côte d'Ivoire inajivunia bidhaa yake ya Cacao katika soko la Uingereza na kuweza kunufaika zaidi kwa kuingiza zaidi mabilioni ya Pauni ya Uingereza (GBP).

Côte d'Ivoire ni mzalishaji mkubwa zaidi wa zao la Cocoa duniani.

Uingereza inaona kwamba kujiondoa katiak Umoja wa Ulaya, haitasumbuka kutokana na kuwa bado ina ushirikiano mzuri na nchi nyingi za Afrika katika masuala ya uchumi, hususan Côte d'Ivoire.

Barani Afrika, nchi kumi na tatu tayari zimesaini mikataba kama hayo na London. Kwa nchi kama Misri na Kenya, soko la Uingereza linaingiza mabilioni ya dola kila mwaka.

Kwa upande wa Nigeria au Afrika Kusini, uchumi wao unategemea Soko la Hisa la London. Brexit haitozuia wingi wa mitaji ambayo Afrika inahitaji kwa maendeleo yake.

Badala yake, inaweza kuimarisha, kwani London inahitaji washirika wapya zaidi kuliko hapo awali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.