Pata taarifa kuu

DRC: Kambi ya Kabila yanzisha vita ya kisheria dhidi ya kufukuzwa kwa Jeanine Mabunda

Wiki moja iliyopita, Wabunge katika ngazi ya taifa nchini DRC walimtimuwa psika wa bunge la kitaifa, Jeanine Mabunda, pamoja na ofisi kuu ya bunge hilo.

Rais wa zamani wa DRC, Joseph Kabila.
Rais wa zamani wa DRC, Joseph Kabila. Kenny Katombe/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Lakini wafuasi wa Rais wa zamani Joseph Kabila wanashtumu utaratibu uliotumiwa ambao wanabaini ulikubwa na ufisadi.

 

Kulingana na vyanzo kutoka kambi ya Joseph Kabila kila mbunge alipewa dola Elfu 10 hadi Elfu 20,000 ili kuweza kupiga kura ya kumtimuwa spika wa Bunge kwenye wadhifa wake na kubaini kwamba zoezi lote hilo liligharimu dola Milioni 15.

 

Kulingana na NOGEC, ufisadi uliathiri sana uchaguzi wa Januari 10. Chama hicho miongoni mwa vyama vinavyounda muungano wa FCC waJoseph Kabila kimebaini kwamba wameambatanisha kwenye faili iliyowasilishwa katika ofisi ya mashitaka video ambazo wabunge kadhaa wanakiri kupokea rushwa.

 

NOGEC imemuomba mwendesha mashtaka kushughulikia haraka kesi hiyo na kuwawikisha mbele ya majaji wwote waliohusika bila kuwa na upendeleo wowote. Kiongozi wa chama hicho, Constant Mutamba ametaka wahusika wote wakamatwe "ili iwe fundisho". Amesema, kashfa hii "inaitumbukiza nchi shimoni". Amesema anasubiri kuona haki imetendeka ili kubaini mafisadi na wafadhili wa mpango huo.

 

Kwa upande wake, Simon Kalenga, msemaji wa chama cha UDPS cha Felix Tshisekedi amefutilia mbali madai hayo akibaini kwamba video zinazosambaa katika mitandao ya kijamii, ni uzushi mtupu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.