Pata taarifa kuu
SUDAN-SIASA

Sudan: Serikali yafuta zaidi ya pasipoti 3,500

Tangu kuanguka kwa utawala wa Omar al-Bashir nchini Sudan, utawala mpya umekuwa ukichunguza tena mfumo wa kupata vitambulisho vya kraia uliofanywa kwa miaka thelathini chini ya utawala wa zamani.

Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok
Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok AP / File Photo
Matangazo ya kibiashara

Pasipoti nyingi ziltolewa kwa maslahi ya kisiasa, kidiplomasia au kifedha.

Kulingana na vyanzo rasmi pasipoti zimefutwa nchini Sudan kwa sababu ya usalama au mgogogoro wa kiafya kwa watu waliozipewa, au kwa sababu hati hiyo ilinunuliwa kwa udanganyifu.

Hii ni operesheni ya kusafisha mfumo wa uraia inayoendelea, ambayo ulianza mwezi Mei 2019, mwezi mmoja baada ya Omar al-Bashir kutimuliwa mamlakani.

Kamati iliundwa kuchunguza maelfu ya pasipoti zilizotolewa chini ya utawala wa zamani, lakini zoezi hilo linakumbwa na visa vya unyanyasaji.

Viongozi wenye ushawishi, kwa mfano, wamekuawa wakiruhusu pasipoti kutolewa baada ya kupokea hongo ya dola Elfu 10 hadi Elfu.

Uraia wa Sudan pia ulikuwa ukipewa wanamgambo wa Kiislam wa upinzani kama vile Tunisia Rached Ghannouchi, mwanzilishi wa chama cha Ennahdha.

Mwaka mmoja uliopita, Baraza Kuu lilitangaza kwamba hati za kusafiria, wakati mwingine za kidiplomasia, zilitolewa kwa viongozi wa makundi ya wanamgambo wa Kiislam wenye msimamo mkali.

Utawala wa zamani pia ulishirikiana vizuri kwa waanchi wa Syria: Wasyria 250,000 walipewa hifadhi ya ukimbizi nchini Sudan tangu mwaka 2011.

Wengi walipata uraia. Omar al-Bashir aliwaruhusu kuomba uraia miezi sita tu baada ya kuwasili kwao Sudan, moja ya nchi adimu kutowazuia kuingia nchini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.