Pata taarifa kuu
SUDAN-SIASA-USALAMA

Sudan: Mvutano waibuka kati ya raia na wanajeshi juu ya taasisi mpya ya kisiasa

Mvutano unaendelea kutokota nchini Sudan kati ya wanajeshi na raia wanaohusika na kuongoza mabadiliko ya kisiasa, siku chache baada ya serikali ya Sudan kufikia mkataba wa amani na waasi.

Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok
Waziri Mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok AP / File Photo
Matangazo ya kibiashara

Jenerali Abdel Fattah al-Burhan ameamua mwenyewe kulipa uwezo mkubwa Baraza la Washirika wa Mpito, taasisi mpya iliyoundwa baada ya makubaliano ya amani na waasi.

Agizo hilo la rais haliijachapishwa hata kwenye Gazeti la serikali au kutangazwa hadharani. Nakala iliyosainiwa na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan ilifichuliwa katika vyombo vya habari siku ya Alhamisi.

Baraza hili la washirika wa Mpito (CPT) hapo awali lilitarajiwa kujikita kwa kazi ya ushauri. Lakini, mkuu wa Baraza Kuu ameamua vinginevyo. Baraza hilo kwa sasa linaweza kuingilia kati hatua za serikali na kuunda bunge lijalo.

Haya ni mapinduzi ya jeshi, vimelaani vyama vya kisiasa na vyama ambavyo viliongoza maandamano dhidi ya Bashir.

Hali ambayo pia inazua sintofahamu ni uteuzi wa kaka wa Hemeti, kiongozi nambari 2 wa sasa wa Baraza Kuu. Ndugu hao wawili wanaongoza Vikosi vya Usaidizi wa Haraka, vikosi vilivyoshtumiwa kutekeleza ukatili na ukandamizaji dhidi ya maamndamano.

Kwa sababu zote hizi, serikali ya kiraia inabaini kwamba agizo hili ni kinyume na tangazo la kikatiba lililopitishwa mnamo mwezi wa Agosti 2019.

Naye Waziri Mkuu Abdallah Hamdok mwenyewe amebaini kwamba Jenerali al-Burhan amekwenda mbali na mamlaka yake kwa kulipa uwezo Baraza hilo mpya la Washirika wa Mpito.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.