Pata taarifa kuu
NIGERIA

WHO: Homa ya Manjano yaua watu 172 nchini Nigeria

Shirika la Afya duniani WHO linasema kuwa homa ya manjano imesababisha vifo vya watu 172 nchini Nigeria, tangu mwaka 2017 ilipoanza kukabiliana na ugonjwa huo, huku watu wengine zaidi ya 500 wakiambukizwa.

Maofisa wa afya wa Nigeria.
Maofisa wa afya wa Nigeria. Simon Akam/Reuters
Matangazo ya kibiashara

Watalaam wa WHO wanaonya kuwa maambukizi ya homa hiyo yanaleta changamoto kubwa kwa taifa hilo la Afrika Magharibi linaloendelea kukabiliana na janga la Corona.

Majimbo yaliyoathiriwa zaidi ni pamoja na Delta, Enugu, Bauchi, Benue na Ebonyi.

 

Kwa mujibu wa tafiti za kisayansi kuhusu ugonjwa wa homa ya manajano, binadamu anapata maradhi hayo baada ya kuumwa na mbu mwenye virusi. Mbu hao wako katika sehemu za joto, barani Afrika na Amerika ya Kusini.

 

Ikiwa mtu anaambukizwa virusi vya ugonjwa huo, ini lake pamoja na viungo vingine vya ndani vinaweza kudhurika na kusababisha kifo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.