Pata taarifa kuu
GHANA

Wagombea urais Ghana watia saini mkataba wa kudumisha amani kuelekea Uchaguzi Mkuu

Wagombea urais nchini Ghana wakiongozwa na rais Nana Akufo-Addo na mpinzani wake mkuu, rais wa zamani John Mahama, wametia saini mkataba wa kudumisha amani, kuelekea Uchaguzi Mkuu siku ya Jumatatu, wiki ijayo.

Rais wa Ghana, Nana Addo akisalimiana na mpinzani wake John Mahama
Rais wa Ghana, Nana Addo akisalimiana na mpinzani wake John Mahama RFI
Matangazo ya kibiashara

Ghana imekuwa ikishuhudia uchaguzi wa utulivu kwa kipàindi kirefu lakini ka,peni za mwaka huu zimeshuhudia kile kinachoelezwa kuwa vitisho kati ya wafuasi w arais Akufo Addo na Mahakama.

Wagombea hao wawili wameaahidi kuhehsimu matokeo ya Uchaguzi huo.

Akufo-Addo mwenye miaka 70, anawania awamu ya tatu na inawezekana kuwa awamu yake ya mwisho.

Kampeni kutoka vyama vyote vikuu vya kisiasa imejikita katika suala la ubunifu wa ajira

Ripoti ya hivi karibuni iliyotolewa na Benki ya dunia inaweka kiwango cha ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana (kati ya miaka 15-24) katika asilimia 48 .

Chama cha NPP kilianzisha kampeni yao mapema mwezi Oktoba kikiwa na manifesto inayosema "Ajenda kwa ajili ya ajira, kubuni fursa na mafanikio kwa wote)."

Wakati wa kampeni , chama cha DPP kimeweza kujenga kiwanda katika kila wilaya zote 216 za Ghana kama njia ya kubuni ajira.

Huku chama cha rais aliyeko madarakani kitoa ilani yake kama "Kubadilisha maisha , kuibadilisha Ghana,"kwa ajili ya Ghana ni ''ajira za kudumu kupitia viwanda''.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.