Pata taarifa kuu

UN: "Janga la kibinadamu nchini Msumbiji limechochewa na ugaidi

Katika mkoa wa Cabo Delgado, Kaskazini mwa Msumbiji unaendelea kukabiliwa na mashambulizi ya makundi ya wanamgambo wa kiislamu kwa miaka mitatu sasa.

Mwanamke mmoja akiwa amebeba mtoto wake, kwenye kijiji kimoja kilichoshambuliwa na wanajihadi wa kiislamu mwaka 2019
Mwanamke mmoja akiwa amebeba mtoto wake, kwenye kijiji kimoja kilichoshambuliwa na wanajihadi wa kiislamu mwaka 2019 AFP/Marco Longari
Matangazo ya kibiashara

Kundi linalodai kuwa la Islamic State limeendelea kuhujumu raia wa mkoa huo, huku wengi wakilazimika kuyatoroka makaazi yao.
 

Hali ya usalama imeendelea kuzorota katika mkoa wa Cabo Delgado katika wiki za hivi karibuni. Idadi ya watu waliokimbia makazi yao imezidi 350,000, na idadi ya vifo vya raia tayari ni mara mbili zaidi ya mwaka 2019.

akihojiwa na François Mazet wa kitengo cha RFI kanda ya Afrika (RFI Afrique), Mjumbe maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Msumbiji Mirko Manzoni, amesema Umoja wa Mataifa unahangaishwa na kudorora kwa usalama nchini Msumbiji na ameomba hatua kali zichukuliwe kukabiliana na zimwi hili la mauaji.

Hata hivyo amebaini kwamba "janga la kibinadamu nchini Msumbiji limechochewa na ugaidi unaoendelea nchini humo.

Katibu Mkuu wa Umoja aw Mataifa alitangaza mnamo Julai 8, 2019 uteuzi wa Mirko Manzoni, raia Uswisi, kama Mjumbe wake Binafsi nchini Msumbiji. Bw. Manzoni ana jukumu la kuwezesha mazungumzo kati ya serikali ya Msumbiji na chama cha upinzani cha RENAMO, kwa lengo la kutia saini kwenye mkataba, na kisha utekelezaji wa makubaliano ya amani kati ya pande hizo mbili hasimu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.