Pata taarifa kuu
NIGERIA

Umoja wa Mataifa walaani mauaji dhidi ya raia 110 Nigeria

Umoja wa Mataifa umesema kuwa watu 110 wameuawa Kaskazini Mashariki mwa Nigeria kufuatia mauaji dhidi ya wakulima, mwishoni mwa wiki iliyopita.

Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari.
Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari. © Nigeria Presidency
Matangazo ya kibiashara

Mauaji hayo yalitokea Jumamposi iliyopita katika kijini cha Koshobe na kijiji kingine cha Jera karibu na mji wa Maiduguri katika jimbo la Borno.

Ripoti zinasema kuwa watu waliokuwa kwenye pikipiki waliwashambulia wanaume na wanwake waliokuwa wakivuna mashambani.

Mbali na mauji hayo ya watu 110; wengine walijeruhiwa na Umoja wa Mataifa unahofia kuwa, huenda kuna wanawake walitekwa.

Hakuna aliyedai kuhusika na shambulizi hilo, lakini kundi la kigaidi la Boko Haram na lile la Islamic State katika eneo la Afrika Magharibi, ISWAP, katika miaka ya hivi karibuni, yalikuwa yakidaiwa kuhusika na mauji kama haya.

Rais Muhammadu Buhari ambaye yuko madarakani tangu mwaka 2015 ameelani mauaji haya ya raia wasiokuwa na hatia na amekuwa akiahidi kupambanana wale wote wanaohusika na mauji nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.