Pata taarifa kuu
DRC

DRC: Waathiriwa wa ubakaji katika gereza la Lubumbashi walalama

Karibu wanawake hamsini waliobakwa katika gereza la Kasapa huko Lubumbashi bado wanasubiri kupata huduma za matibabu.

Wanawake mjini Lubumbashi, wakiandamana kupinga ukatili kwenye jimbo la Haut-Katanga.
Wanawake mjini Lubumbashi, wakiandamana kupinga ukatili kwenye jimbo la Haut-Katanga. Rfi/Denise Maheho
Matangazo ya kibiashara

Wanawake hawa walishikiliwa katika gereza la Kasapa wakati wa ghasia zilizozuka katika gereza hilo mnamo Septemba 25, 26 na 27.

Tangu wakati huo, hawajakutana na daktari yoyote wa wanawake au afisa wa ofisi ya mashitaka ili aweze kwasikiliza yaliyowasibu. Wameendelea kuelezea masikitiko yao kuona serikali haiwajali.

RFI imeweza kukutana nao katika sehemu ndogo waliojengewa katika jela hilo la Kasapa. Hapo ndipo wanalala usiku na watoto wao. Sehemu walikokuwa wanazuiliwa ilichomwa moto, sawa na zile za wanaume wakati wa ghasia.

Wanawake hao wameebaini kwamba walibakwa kwa siku tatu mfululizo, (Septemba 25, 26 na 27), baadhi wakibakwa karibu na wafungwa ishirini.

Umoja wa Matiafa pia unasema ulipata ripoti za kuaminika kwamba wavulana na wasichana wa chini ya umri 18 walifanyiwa kitendo hicho cha kinyama.

Waathiriwa wamesema walikuja kupata afueni wakati mamlaka ilichukua udhibiti wa gereza mnamo Septemba 28.

Wanawake hao wanasema tangu wakati huo, hawajapewa huduma yoyote ya matibabu, ispokuwa dawa zilizotupa muda za kupunguza makali ya ukimwi na vifaa 20 vya matibabu ndivyo walivyopewa tu.

Wataalam wanasema dawa hizo ni ndogo na muda umesha kuwa mrfeu, kwa wamechelewa kupewa matibabu ya kutosha. Wanawake hawa wako katika hatari ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa, kupata ujauzito na kupata matatizo ya kiafya.

Wanawake hao wameongeza kwamba kwa sasa wanasumbuliwa na maumivu ya tumbo na damu zisizokata. Wengi wa wanawake hawa hawajasikilizwa na majaji.

Wengine wanazuiliwa kwa makosa madogo, kama vile afisa wa polisi wa miaka 60 aliyefungwa kwa kupoteza kofia yake na msichana anayedai kuwa amefungwa baada ya mgogoro na mke wa baba yake.

Wakati huo huo kampeni ya siku 16 za kukomesha Ukatili wa Kijinsia inaendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Wanaharakati wa haki za binadamu wanasemawanawake hao wamesahaulika kabisa, wakiiomba serikali kuwatendea haki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.