Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA-HAKI

DRC: Kiongozi wa wanamgambo Sheka ahukumiwa kifungo cha maisha

Mahakama ya kijeshi Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), imemhukumuT abo Taberi kwa jina maarufu Sheka, kiongozi wa zamani wa kundi la wanamgambo wa Nduma Defence of Congo (NDC), kifungo cha maisha jela, kwa uhalifu uliofanywa kati ya mwaka wa 2009 na 2014.

Wilaya ya Walikale, Kivu Kaskazini. Maandamano ya amani katika sehemu ya mazungumzo ya kijamii, mkutano wa siku tatu ambao ulileta pamoja zaidi ya washiriki 300 kutoka maeneo 16 katika wilaya ya Walikale, mnamo Desemba 2019.
Wilaya ya Walikale, Kivu Kaskazini. Maandamano ya amani katika sehemu ya mazungumzo ya kijamii, mkutano wa siku tatu ambao ulileta pamoja zaidi ya washiriki 300 kutoka maeneo 16 katika wilaya ya Walikale, mnamo Desemba 2019. MONUSCO/ Alain Wandimoyi K
Matangazo ya kibiashara

Tabo Taberi Cheka, amehukumiwa kifungo cha maisha jela pamoja na washtakiwa wengine wawili kufuatia uhalifu unaohusiana na mauaji, utumwa wa kingono na kuwaingiza watoto jeshini, uchomaji moto baadhiya vijiji katika Wilaya ya Walikale katika mkoa wa Kivu Kaskazini kati ya mwaka wa 2009 na 2014.

Waathiriwa 337 waliotambuliwa na ushahidi uliotolewa vimepelekea majaji wa Mahakama ya kijeshi kuchukuwa uamuzi: mwanzilishi wa kundi la Nduma Defence of Congo (NDC) na naibu wake, Séraphin Zitonda, anayejulikana kama kamanda katika kundi la waasi wa Kihutu wa Rwanda (FDLR), wamehukumiwa kifungo cha maisha. Mwanajeshi mwingine amehukumiwa kifungo cha miaka kumi na tano. Mshtakiwa wa nne ameachiliwa huru, ni mtoto ambaye aliingizwa kwa nguvu katika kundi hilo.

Majaji wamekumbusha ushuhuda wa mtoto aliyesajiliwa kwa nguvu akiwa na umri wa miaka 9 baada ya mauaji ya familia yake yote na wanamgambo hao.

Wakati kesi hiyo ikisikilizwa mahakamani, mtoto huyo alimkabili Sheka, akimshtumu "kuiba" utoto wake.

Upande wa tume ya umoja wa mataifa nchini Congo DRC umeridhika na hukumu hiyo dhidi ya viongozi hao wa waasi , na kuwa na matumaini ya kurejea kwa usalama nchini Mashariki mwa DRC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.