Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-UCHAGUZI-SIASA-USALAMA

Burkina Faso: Upinzani watoa onyo dhidi ya 'matokeo yaliyogubikwa na udanganyifu'

Upinzani nchini Burkina Faso umeituhumu tume ya uchaguzi kwa kushindwa kufungua vituo vya kupigia kwa wakati, na kusema kuwa hautakubali matokeo yoyote kufuatia kile unachokisema kumekuwepo na udanganyifu wa kura.

Tahirou Barry, Ablassé Ouédraogo, Zéphyrin Diabré na Eddie Komboïgo, wagombea urais nchini Burkina Faso, katika taarifa ya awali, Novemba 21, 2020.
Tahirou Barry, Ablassé Ouédraogo, Zéphyrin Diabré na Eddie Komboïgo, wagombea urais nchini Burkina Faso, katika taarifa ya awali, Novemba 21, 2020. © Paulina Zidi/RFI
Matangazo ya kibiashara

Tume ya Uchaguzi imesitisha zoezi la kutangaza matokeo ya awala kutoka kwa kila wilaya, kama ilivyoanza kufanya tangu Jumatatu adhuhuri.

Hatua hiyo imekuja baada ya taarifa kutoka kwa wagombea saba waliosaini makubaliano ya kisiasa ambao walitoa walitoa onyo dhidi yaTume ya Uchaguzi, CENI. Wameelezea pia "kutoridhishwa kuhusu ukweli na uaminifu wa matokeo ya uchaguzi", wakilaani "udanganyifu mkubwa uliogubika na kasoro zilizojitokeza kwenye zoezi hilo".

Katika taarifa iliyosomwa na Tahirou Barry, mkutano wa wagombea wa upinzani unalaani "usimamizi wa CENI katiak uchaguzi" na maanfdalizi mabaya ya uchaguzi."

Ni wazi kuwa vituo vya kupigia kura vilivyopangwa kufunguliwa viliendelea kufungwa wakati vituo vingine ambavyo havikutakiwa kufunguliwa kwa sababu za ukosefu wa usalama vilifunguliwa dakika ya mwisho bila mashauriano na wanasiasa wote na bila idhini ya Mahakama ya Katiba kama inavyotakiwa. Kwa hivyo upinzani haukuweza kushiriki katika ufuatiliaji wa shughuli za uchaguzi katika vituo hivi vya kupigia kura, "Tahirou Barry amewaambia waandishi wa habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.