Pata taarifa kuu
LIBYA-WAHAMIAJI-USALAMA

Wahamiaji wengine 20 wakufa maji katika pwani ya Libya

Wahamiaji wengine zaidi ishirini wamepoteza maisha baada ya boti lao kulizama katika pwani ya Libya, shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limetangaza leo Ijumaa, siku moja baada ya ajali nyingine mbaya kugharimu maisha ya wahamiaji wasiopungua 74.

Wavuvi na kikosi cha walinzi wa baharini wamepata miili 31 kutoka boti la kwanza lililozama siku ya Alhamisi, ikiwa ni pamoja na mwili wa mtoto mdogo.
Wavuvi na kikosi cha walinzi wa baharini wamepata miili 31 kutoka boti la kwanza lililozama siku ya Alhamisi, ikiwa ni pamoja na mwili wa mtoto mdogo. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Boti hilo likuwa limetokea katika mji wa Surman, magharibi mwa mji mkuu wa Libya, Tripoli.

Kwa jumla, watu wasiopungua 94 wamepoteza maisha katika ajali hizi mbili za boti, amesema msemaji wa shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM).

"Wafanyakazi wetu katika eneo hilo wameripoti kwamba miili mingine ya wahamiaji ilionekana usiku katika pwani ya Libya," Safa Msehli amesema katika mkutano na waandishi wa habari huko Geneva, nchini Uswisi.

Wavuvi na kikosi cha walinzi wa baharini wamepata miili 31 kutoka boti la kwanza lililozama siku ya Alhamisi, ikiwa ni pamoja na mwili wa mtoto mdogo.

Manusura wanashikiliwa katika mji wa Khoms nchini Libya, msemaji huyo ameongeza, akitoa wito kwa mamlaka kuwaachilia na kuwapa ulinzi ili kuwazuia wasijikute mikononi mwa wafanyabiashara haramu wa binadamu.

Zaidi ya watu 900 wamekufa mwaka huu wakijaribu kuvuka Bahari ya Mediterania ili kuingia Ulaya. Maelfu zaidi walikamatwa baharini na kurudishwa Libya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.