Pata taarifa kuu
DRC-RWANDA-CORONA-BIASHARA-UCHUMI

Biashara ndogo ndogo ya mpakani yaanza hatua kwa hatua kati ya Rwanda na DRC

Mpaka kati ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Rwanda ulifungwa mnamo mwezi Machi mwaka huu kwa sababu ya mgogoro wa kiafya, uliyotokana na Corona.

Eneo la mpaka kati ya DRC na Rwanda.
Eneo la mpaka kati ya DRC na Rwanda. REUTERS/Djaffer Sabiti
Matangazo ya kibiashara

Katika siku za hivi karibuni, viongozi wa DRC na Rwanda wamekubalia kuruhusu makundi kadhaa ya watu kuvuka mpaka kwenye maeneo manne ya mipakani kati ya nchi hizo.

Lengo ni kuwezesha biashara na kupunguza shida za kiuchumi zinazowakabilia wakaazi wa maeneo hayo ya mipakani.

Shughuli kwenye maeneo ya mipaka ya Bugavu na Goma zilianza tena Novemba 5.

Wakaazi wa maeneo hayo ya mipakani wamekaribisha hatua hiyo ya viongozi wa nchi hizo mbili na kubaini kwamba wataheshimu masharti yaliyowekwa na mamlaka kutoka nchi hizo.

"Nina furaha kubwa kuweza kuvuka tena mpaka. Narudi kufanya tena shughuli yangu kama kawaida, hivi sasa naona kuwa nirudi kuwa na maisha kama yale ya kabla ya kuzuka kwa janga la Corona, " amesema Ramedi Bizimana, mmoja wa wanachama wa shirika la wachukuzi wa mpakani kutoka Rubavu nchini Rwanda.

Kabla ya janga la Corona, wakaazi kutoka maeneo hayo ya mpakani walikuwa wakivuka mpaka mara kadhaa kwa siku baada tu ya kuonyesha kitambulisho cha uraia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.