Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-SIASA-USALAMA-HAKI

Serikali ya Côte d’Ivoire yafungua mashitaka mahakamani baada ya kuundwa kwa CNT

Serikali ya Côte d’Ivoire imefikish malalamiko yake mbele ya mahakama kutokana na wito wa upinzani kukaidi shughuli za serikali na kuundwa kwa baraza la Kitaifa la Mpito, CNT. Serikali imetangaza uamuzi huo mapema mchana. Wakati huo huo vikosi vya usalama vimepiga kambi mbele ya makaazi ya 'Henri Konan Bédié.

Polisi wakipiga kambi mbele ya nyumba ya Henri Konan Bédié huko Abidjan, Côte d'Ivoire, Novemba 3, 2020.
Polisi wakipiga kambi mbele ya nyumba ya Henri Konan Bédié huko Abidjan, Côte d'Ivoire, Novemba 3, 2020. RFI/Benjamin Avayou
Matangazo ya kibiashara

Polisi iliwataka waandishi wa habari waondoke wakati walikuwa wakisubiri mkutano na kiongozi huyo wa upinzani, kabla ya kuzingira nyumba yake.

Hali ni ya kutatanisha mbele ya makaazi ya Bédié.

Mapema Jumanne wiki hii, katika taarifa kwa vyombo vya habari, serikali ya Côte d’Ivoire ililaani uundwaji wa Baraza la Kitaifa la Mpito, CNT, lililotangazwa na upinzani, Jumatatu alaasiri.

Kulingana na serikali tangazo hilo pamoja na machafuko yatakayotekelezwa kufuatia wito huo wa kukaidi shughuli za serikali ni “vitendo vya mashambulizi na kula njama dhidi yamamlaka ya nchi na uhuru wa taifa”.

waziri wa Sheria, Sansan Kanbile, ametangaza kwamba tayari wamefikisha malalamiko yao kwa mwendesha mashitaka na kwenye mahakama ya mwanzo ili wahusika wafikishwe mahakamani.

Cette déclaration ainsi que les violences perpétrées suite au boycott actif constituent des actes d’attentat et de complot contre l’autorité de l’État et l’intégrité du territoire national.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.