Pata taarifa kuu
SUDAN-MAREKANI-USHIRIKIANO

Donald Trump aongeza vikwazo dhidi ya Sudan kwa mwaka mmoja

Katika uamuzi ambao haukutarajiwa saa chache kabla ya uchaguzi wa urais nchini Marekani, Rais Donald Trump ametia saini agizo rasmi jioni ya Jumatatu, Novemba 2, ikiongeza muda wa vikwazo dhidi ya Sudan kwa mwaka mwingine.

Rais wa Marekani Donald Trump katika ofisi yake, White House.
Rais wa Marekani Donald Trump katika ofisi yake, White House. REUTERS/Jonathan Ernst
Matangazo ya kibiashara

Sudan iliwekwa na Marekani kwenye orodha yake nyeusi ya nchi zinazo unga mkono ugaidi.

Kulingana na taarifa ya Ikulu iliyosainiwa na Donald Trump, licha ya Khartoum kupiga hatua kubwa hivi karibuni, mgogoro uliotokea kutokana na vitendo na sera za serikali ya Sudan ambavyo vilisababisha kuchukuliwa vikwazo mbali mbali tangu mwaka 1997, "bado havijatatuliwa ”.

Taarifa hiyo imebaini vitendo na sera hizo "zinaendelea kuwa tishio lisilo la kawaida na maalum kwa usalama wa kitaifa wa Marekani na sera za kigeni."

Kutokana na hali hiyo, rais wa Marekani aliamua Jumatatu jioni kuwa ni lazima kuongezea tena muda wa mwaka mmoja vikwazo dhidi ya Sudan.Kwa amri hiyo hiyo, Donald Trump pia ameongeza muda wa hali ya hatari iliyotangazwa na Marekani mnamo mwaka 1997 dhidi ya Sudan kutokana na hali ya Darfur.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.