Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

Serikali ya DRC yaanza mashauriano kumaliza mvutano wa kisiasa unaoendelea

Mashauriano yaliyotangazwa na rais Tshisekedi yanaanza Jumatatu hii, Novemba 2. Mikutano mifupi, ambayo ikulu ya rais imebaini kwamba ingelipenda isichukuwi siku nyingi, inalenga kumaliza mkwamo wa shughuli za serikali kutokana, kulingana na Felix Tshisekedi, na tofauti za maoni na mwenzake, Joseph Kabila, na muungano wake, FCC.

Rais wa DRC Félix Tshisekedi alitangaza mashauriano kwa nia ya "umoja wenye kudumu".
Rais wa DRC Félix Tshisekedi alitangaza mashauriano kwa nia ya "umoja wenye kudumu". Mikhail Metzel / SPUTNIK / AFP
Matangazo ya kibiashara

Siku hii ya kwanza ya mashauriano itagubikwa kwa kiasi kikubwa kwa maswali ya uchaguzi.

Uteuzi wajumbe wa tume ya uchaguzi, mageuzi yaliyotakiwa kufanywa na hata uchaguzi wa mgombea atakaye uungwa mkono kwa uchaguzi wa urais wa mwaka 2023, ni baadhi ya sababu za mgawanyiko kati ya miungano ya CACH na FCC.

Maafisa wa Tume Huru ya Uchaguzi, CENI, wanaomaliza muda wao ni miongoni mwa wadau wa kwanza wataanza kuhiriki mashauriano hayo. Kutakuwa pia na wawakilishi wa mashirika maalumu katika masuala haya, kama vile Symocel au AETA. Au wawakilishi wa dini mbalimbali kama wale wa Kanisa la Kristo nchini DRC. Hata hivyo, Baraza Kuu la Maaskofu, CENCO, ambalo linahusika kwa kiasi kikubwa katika maswali haya, linapendelea kushiriki vikao hivyo baadaye.

Felix Tshisekedi ameendelea kushutumu mkwamo wa shughuli za serikali unaosababishwa na mungano wa FCC wa Joseph Kabila na kambi yake. Inasemekana kwamba rais wa DRC anatafuta muungano mpya. Anaweza hata kuanza kukutana na wanasiasa Jumanne wiki hii, mmoja wa washauri wake amebaini, huku akieleza kuwa rais Tshisekedi anataka kusikiliza maoni tofauti juu ya maswala muhimu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.