Pata taarifa kuu
LIBYA-UN-USALAMA-SIASA

UN: Tuna imani na kufikiwa kwa mkataba wa kudumu wa kusitishwa kwa mapigano Libya

Kaimu mwakilishi wa Umoja wa Mataifa kwa nchi ya Libya, Stephanie Williams, amesema ana imani ya kufikiwa kwa mkataba wa kudumu wa kusitisha mapigano nchini Libya kutokana na mazungumzo yanayoendelea kati ya pande hasimu.

Kaimu mwakilishi wa Umoja wa Mataifa kwa nchi ya Libya, Stephanie Williams.
Kaimu mwakilishi wa Umoja wa Mataifa kwa nchi ya Libya, Stephanie Williams. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Pande hizo tayari zimefikia makubaliano juu ya kufunguliwa tena kwa safari za anga na nchi kavu.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari huko Geneva, mwanadiplomasia huyo kutoka Marekani amesema pande hizo mbili, ambazo zinajadiliana huko Geneva wiki hii, pia zimekubaliana kudumisha "utulivu katika maeneo ya vita na kuepusha kuongezeka kwa mapigano".

Serikali ya umoja aw kitaifa , yenye makaazi yake mjini Tripoli, ambayo inatambuliwa na jamii ya kimataifa, na wapiganaji wa kundi la LNA) linaloongozwa na Marshal Khalifa Haftar, mbabe wa kivita mashariki mwa Libya, wanapigania udhibiti wa Libya kwa miaka kadhaa, kwa usaidizi wa nchi za kigeni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.