Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Hali ya wasiwasi yatanda Mikenge, DRC

Watu kutoka jamii mbalimbali katika kijiji cha Mikenge, katika mkoa wa Kivu Kusini, Mashariki mwa DRC, wameendelea kulaumiana kila upande kuunga mkono makundi yenye silaha.

Karibu Banyamulenge 3,000 waliotoroka makazi yao bado ni wakimbizi karibu na kambi ya MONUSCO huko Mikenge.
Karibu Banyamulenge 3,000 waliotoroka makazi yao bado ni wakimbizi karibu na kambi ya MONUSCO huko Mikenge. Sonia Rolley/RFI
Matangazo ya kibiashara

Kwenye Milima ya Minembwe, kuna maelfu ya wakimbizi, waliokimbilia karibu na kambi za kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO, na hawana msaada wa kimataifa.

Katika kijiji hiki cha Mikenge kuna karibu wakimbizi 3,000, hasa watu kutoka jamii ya Banyamulenge, na wanasema walikumbwa na mashambulizi mengi.

Wakihojiwa na Sonia Rolley, mwandishi wa RFI, wakimbizi hao wamesema wameshambuliwa mara ishirini na wanawajua waliotekeleza mashambulizi hayo. Philemon Chiza, mmoja wa wawakilishi wao, amesimulia shambulio la hivi karibuni la mwezi Julai. “Nitawaonyesha walikotokea. Wapiganaji wa kundi la Mai-Mai walitokea kwenye mlima huu, kwa njia hii. Waliingia kambini, wakafyatua risasi. MONUSCO ilijaribu kukabiliana nao. Askari kadhaa walijeruhiwa.

Hata hivyo Philemon Chiza amebaini kwamba anawajua wapiganaji hao wa kundi la Mai-Mai waliotekeleza shambulio hilo: "Ndio, ni watu kutoka hapa, kutoka kijiji hiki. Mvulana aliyepoteza maisha hapa, baba yake bado yuko hapa. "

Katika vijiji jirani vinavyokaliwa na jamii hasimu za Banyamulenge, wanakanusha kuwa na uhusiano na makundi ya Mai-Mai. Kijana mmoja kutoka jamii ya Wafulero anawatuhumu wakimbizi hao kutoka jamii ya Wanyamulenge kwa kuunga mkono waasi wa Banyamulenge au hata kuwa na silaha. “Silaha zimefichwa pale kunakopatikana vibanda vidogo. Akihojiwa kuhusu alijuaje kuwa silaha zimefichwa sehemu hiyo, alijibu: “Tuliziona wakati FARDC ilikuja kufanya msako na kuzikamata. "

Kwenye Milima ya Minembwe, wengi wamemzungumzia Kanali Michel Rukunda, anayejulikana kwa jina la Makanika, aliyeasi jeshi la DRC ambaye sasa anaongoza sehemu ya makundi yenye silaha ya Banyamulenge. Uwepo wake umeripotiwa karibu kilomita 20 kutoka kambi ya wakimbizi wa ndani ya Mikenge.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.