Pata taarifa kuu
MALI-SIASA-USALAMA

Mali: Serikali mpya ya mpito yatangazwa, jeshi lashikilia nafasi muhimu

Serikali ya mpito nchini Mali imetangazwa. Kati ya mawaziri 25, wanajeshi wanashikilia nyadhifa nne muhimu: Ulinzi, Usalama, Maridhiano ya Kitaifa na Utawala.

Waziri Mkuu wa Mali Moctar Ouane, Septemba 21, 2006, katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Waziri Mkuu wa Mali Moctar Ouane, Septemba 21, 2006, katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa wakati alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. AP Photo/Frank Franklin II, File
Matangazo ya kibiashara

Katika serikali yenye mawaziri 25, jeshi lina nyadhifa nne muhimu: Kanali Sadio Camara ameteuliwa kuwa waziri wa ulinzi, Kanali Modibo Kone ameteuliwa kuwa waziri wa usalama na Kanali Ismael Wague kapewa wizara ya maridhiano ya kitaifa.

Waziri mpya wa Uchumi na Fedha, ni Alousséni Sanou, kada wa benki moja nchini Mali.

Vuguvugu la 5M5, lililoanzisha maandamano na kushiriki katika kuangusha utawala wa zamani na kiongozi wao wa kiroho Imam Mahmoud Dicko wamepewa wizara tatu: Mawasiliano, Wizara ya Ajira inayoshikiliwa na Mohamed Salia Touré , na mwishowe Wizara ya Haki inayochikiliwa na Mohamed Coulibaly, aliye karibu sana na kigogo wa vuguvugu la M5, Cheick Oumar Sissoko.

Wizara ya Mambo ya nje, na ile ya Maswala ya Ardhi, ziko chini ya mamlaka ya Waziri Mkuu, Moctar Ouane.

Wizara ya Kilimo, ilipewa mwakilishi wa kundi la zamani la waasi, Mahmoud Ould Mohamed. Wizara ya Vijana pia inashikiliwa na mmoja wa waasi wa zamani. Wakili Harouna Toureh, mmoja wa viongozi wamakundi yenye silaha yanayounga mkono serikali, ameteuliwa kuwa Waziri wa Kazi na msemaji wa serikali.

Serikali hii ina jumla ya wanawake wanne. Miongoni mwao, Kadiatou Konaré, binti wa Rais wa zamani wa Mali Alpha Oumar Konaré, ambaye amejizolea umaarufu katika uchapishaji, ameteuliwa kuwa Waziri wa Utamaduni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.