Pata taarifa kuu
DRC-MAFURIKO-USALAMA

Sita wafariki dunia katika kijiji cha Sake, Mashariki mwa DRC

Watu sita wamepoteza maisha na mamia hawana makaazi katika eneo la Sake, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kufuata mafuriko makubwa yanayosabishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha.

Wakati juhudi za kutafuta miili ya waliofariki zikiendelea, mashirika ya kiraia kijijini Sake yametoa wito kwa serikali ya DRC kufanya kila jitihada za kuwalinda raia wake.
Wakati juhudi za kutafuta miili ya waliofariki zikiendelea, mashirika ya kiraia kijijini Sake yametoa wito kwa serikali ya DRC kufanya kila jitihada za kuwalinda raia wake. Shube Ngorombi/RFI
Matangazo ya kibiashara

Raia waishio  kijijini sake wasema  kwamba mafuriko hayo yalisababishwa na mvua kubwa.

“Mvua ilinyesha na nyumba nyingi zimeharibiwa, watu  wasiopungua wanane walifariki, “ amesema Bavon Myachi, mmoja wa wakaazi wa Sake.

“Tunataka Baba Tshisekedi atusaidie kama mataifa mengine Ulimwenguni kwani tunateseka, “ amebaini Lukaya Sousan, mkaazi mwengine wa Sake.

Wakati juhudi za kutafuta miili ya waliofariki zikiendelea, mashirika ya kiraia kijijini Sake yametoa wito kwa serikali ya DRC kufanya kila jitihada za kuwalinda raia wake.

“Mto wa Kihira mara kwa mara unasababisha hasara.Tunachohitaji, serikali ihamasishe raia kupanda miti kwa lengo la kuzuia mafuriko kama na hayo, “ amesema Masudi Olivier, kiongozi wa muungano wa vijana kijijini Sake.

Hata hivyo serikali ya Mkoa wa Kivu Kaskazini imeimebaini kwamba inaendelea kufanya uchunguzi na kutafuta suluhisho dhidi ya maafa yanayo zorotesha usalama wa raia wake.

Itakumbukwa kwamba mwaka uliopita Mto wa Kihira ulisababisha vifo vya watu watatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.