Pata taarifa kuu
DRC-TSHISEKEDI-KABILA-SIASA-USALAMA

Felix Tshisekedi na mtanguklizi wake wakutana kujaribu kutatua mvutano kati ya FCC na CACH

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi amekutana na mtangulizi wake Joseph Kabila, katika kikao kinachoamiwa kililenga kutathmini ushrikiano kati ya miungano miwili ya kisiasa ya FCC na CACH inayoongoza serikali.

Joseph Kabila na Félix Tshisekedi bega kwa bega wakati wa hafla ya kuapishwa kwa rais mpya wa DRC, huko Kinshase Januari 24, 2019.
Joseph Kabila na Félix Tshisekedi bega kwa bega wakati wa hafla ya kuapishwa kwa rais mpya wa DRC, huko Kinshase Januari 24, 2019. REUTERS/ Olivia Acland
Matangazo ya kibiashara

Rais Tshisekedi ameendelea kuongoza nchi hii tangu mwaka uliopita, kwa ushirikiano na wabunge na maseneta wa mtangulizi wake, ambao ni wengi.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa watu wa karibu na kabila, mambo kadhaa yalijadiliwa wakati wa kikao hicho, ikiwemo jinsi ya kuendeleza na kuimarisha muungano wa FCC.

Kabla ya mkutano huu, kumeshuhudiwa mvutano kati ya pande hizo mbili kuhusu masuala mbalimbali, hasa uteuzi wa watu wanaohudumu katika nayadhifa za juu serikalini.

Miaka mitatau kuelekea Uchaguzi Mkuu, baadhi ya mawaziri kutoka upande wa muungano wa rais Kabila, wameonesha wazi kuwa wanamtaka rais huyo wa wamani kurejea madarakani.

Waziri wa Mazingira Claude Nyamugabo ameeleza wazi na kusema kuwa anatarajia kuwa Kabila atarejea tena uongozini wakati wa Uchaguzi Mkuu ujao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.