Pata taarifa kuu
MALI-AU-SIASA-USALAMA

AU yaweka shinikizo kwa Mali kwa uteuzi wa raia kuongoza kipindi cha mpito

Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika limeendelea na kuweka shinikizo kwa viongozi wa kijeshi wanaoshikilia madaraka nchini Mali kwa minajili ya kumteua raia watakaongoza nchi hiyo kama rais na waziri wake mkuu katika kipindi cha mpito.

Umoja wa Afrika, kama ECOWAS, wamepinga mwanajeshi kuongozi Mali katika kipindi cha mpito.
Umoja wa Afrika, kama ECOWAS, wamepinga mwanajeshi kuongozi Mali katika kipindi cha mpito. MICHELE CATTANI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Baraza hulo la Amani na Usalama la AU lilikutana katika kmutano kwa njia ya video Alhamisi, Septemba 17. Kama ECOWAS Jumanne wiki hii, Umoja wa afrika unaendelea kudai kwamba kipindi cha mpito nchini Mali kinapaswa kuongozwa na raia.

Rais wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika, Ismaël Chergui, amebaini kwamba viongozi wa kijeshi wanaoshikilia madaraka wanapaswa kufanya uteuzi wa rais ambaye atakuwa kama rais wa nchi hiyo kwa kipindi cha mpito na kuheshimu katiba ya nchi.

Agosti 19, AU ilisiisimamisha Mali kwenye uanachama wa umoja huo baada tu ya mapinduzi.

Au imeungana na Jumuiyaya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika, ECOWAS kwa kutaka kipindi cha mpito kiwe na muda wa miezi 18 na hawataki mwanajeshi kuongoza nchi hiyo kama rais katika kipindi cha mpito.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.