Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-CORONA-UCHUMI

Afrika Kusini kufungua mipaka yake Oktoba 1

Afrika Kusini imetangaza kwamba itafunguwa mipake yake ili kuruhusu kuingia nchini humo wageni kutoka nchi mbalimbali na kuwezesha raia wake kusafiri nje ya nchi ifikapo OKtoba 1. 

Rais aw Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akilihutubia taifa.
Rais aw Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akilihutubia taifa. REUTERS/Sumaya Hisham
Matangazo ya kibiashara

Orodha sahihi ya nchi zinazohusika na vizuizi hivi vilivyowekwa na mamlaka nchini humo itatolewa baadaye, Rais Cyril Ramaphosa amesema katika hotuba yake kwenye televisheni.

Orodha hiyo itatolewa "kulingana na taarifa za hivi karibuni za kisayansi" zilizopo.

Wiki hii utafiti wa watalaam wa afya nchini Afrika Kusini, ulibaini kuwa watu Milioni 12 waliambukizwa virusi vya Corona, katika taifa hilo ambalo limeongoza kwa maambukizi barani Afrika.

Waziri wa Afya wa Afrika Kusini Zweli Mkhize alisema utafiti huo mpya unakadiria kuwa, watu milioni 12 ambao ni sawa na  asilimia 20% ya idadi ya watu nchini humo, huenda tayari wameambukizwa virusi  hivyo, katika nchi hiyo ambayo ina maambukizi zaidi ya Laki Sita.

Utafiti huo unaonesha kuwa idadi halisi ya maambukizi inaweza kuwa kubwa zaidi, kati ya 35% na 40%, na watu waliothirika zaidi ni wale wanoishi katika maeneo ambayo kuna watu wengi.

Hata hivyo, kupungua kwa maambukizi katika siku za hivi karibuni kumezua maswali kuhusu kiwango cha kingamwili kwenye damu ya wagonjwa waliopimwa.

Mwezi Julai, kati ya kesi mpya 10,000 na 15,000 ziliripotiwa kila siku. Lakini katika saa 24 zilizopita, kesi mpya 956 tu ndizo zilizoripotiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.