Pata taarifa kuu
MALI-ECOWAS-SIASA-USALAMA

ECOWAS yatoa muda kwa jeshi kumteua raia kuwa rais wa mpito wa Mali

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, inaendelea na vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Bamako na dhidi ya Kamati ya Kitaifa ya Wokovu wa wananchi (CNSP), wanajeshi waliochukua madaraka baada ya kumpindua rais Ibrahim Boubacar Keïta.

Siku ya kwanza ya mashauriano ya kitaifa, Jumamosi Septemba 5, 2020, Bamako, Mali.
Siku ya kwanza ya mashauriano ya kitaifa, Jumamosi Septemba 5, 2020, Bamako, Mali. David Baché/RFI
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu umechukuliwa katika mkutano wa viongozi wa nchi hizo waliokutana Jumatatu hii Septemba 7 huko Niamey, mji mkuu wa Niger. Mkutano ambao uliangazia hali inayoendelea nchini Mali, baada ya jeshi kupindua aliyechaguliwa Ibrahim Boubacar Keita.

Mkutano huo, ulioongozwa na rais wa Niger, Mahamadou Issoufou, ulimalizika jioni. ECOWAS imeomba wanajeshi wanaoshikilia madaraka nchini Mali kumteua rais, raia, ifikapo Septemba 15.

"Wakati wa mapinduzi katika Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrijka Magharibi, ECOWAS, umekwisha," viongozi hao wamesema katika mkutano huo.

Rais wa sasa wa ECOWAS, Mahamadou Issoufou, ametoa tena wito wa kurejeshwa taasisi za kiraia kuliongoza taifa hilo linalokabiliwa na ukosefu wa kutosha wa usalama kutokana na mashambulizi ya hapa na pale ya makundi yenye silaha, na visa vya utekaji nyara na mauaji.

Kwa kauli moja viongozi wa nchi hizo wameamua kubakiza vikwazo vyote vilivyochukuliwa dhidi ya wanajeshi wanaoshikilia madaraka.

ECOWAS imetoa muda wa wiki moja kwa kwa kundi la wanajeshi hao kumteua rais wa mpito pamoja na Waziri wake Mkuu, ambao wote ni raia. Kwa hivyo, kiongozi mpya wa Bamako ana hadi Septemba 15, 2020 kujibu vyema matakwa ya ECOWAS.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.