Pata taarifa kuu
MALI-UFARANSA-USALAMA

Mali: Ufaransa yawapoteza wanajeshi wake wawili katika Mkoa wa Tessalit

Wanajeshi wawili wa kikosi cha Ufaransa katika eneo la Sahel, Barkhane, wameuawa na mmoja kujeruhiwa vibaya, tukio lililotokea Jumamosi, Septemba 5 asubuhi.

Wanajeshi wa Ufaransa wa kikosi cha Barkhane nchini Mali
Wanajeshi wa Ufaransa wa kikosi cha Barkhane nchini Mali Reuters
Matangazo ya kibiashara

Duru za kuaminika zinabaini kwamba wanajeshi hao waliuawa katika mlipuko wa bomu lililotengenezwa kienyeji katika Mkoa aw Tessalit, kaskazini mwa Mali.

Taarifa kutoka ikulu ya rais wa Ufaransa imetangaza "vifovya wanajeshi wawili wa Ufaransa, Brigadier-Chief First Class ST na Hussar Parachutist First Class Arnaud Volpe, baada ya gari lao la kivita kukanyaga kifaa cha kulipuka (... wakati wa operesheni ”katika mkoa wa Tessalit, kaskazini mwa Mali."

Wanajeshi watatu waliokuwa watatu walikuwa katika gari walijeruhiwa vibaya na walianza kuhudumiwa mara moja", makao makuu ya majeshi ya Ufaransa yametangaza muda mfupi baadaye. Wawili kati ya watatu hao walifariki kutokana na majeraha waliyoyapata na "mwenzaoanaendelea vizuri."

Alikihojiwa na RFI, Kanali Frédéric Barbry, msemaji wa makao makuu ya majeshi ya Ufaransa amebaini kwamba "kufikia sasa, kundi la kigaidi lililotega kifaa hicho cha kulipuka halijatambuliwa na uchunguzi ambao umeanzishwa utabaini ikiwa kifaa hiki cha kulipuka kilitegwa hivi karibuni au hata kabla ya msimu wa mvua."

"Rais wa Jamhuri amepongeza tena ujasiri na dhamira ya wanajeshi wa Ufaransa waliopelekwa katika eneo la Sahel, pamoja na ndugu zao wanajeshi kutoka nchi nyingi zinazohusika kwa pamoja katika ujumbe huu mgumu," imeongeza ikulu ya Elysee katika taarifa yake.

Kulingana na makao makuu ya majeshi ya Ufaransa, idadi hii inafikisha wanajeshi 45 wa Ufaransa waliouawa katika mapigano wakati wa operesheni Serval (2013) na Barkhane (tangu Agosti 2014), ambayo ina wanajeshi 5,000. Mwezi Novemba 2019, Ufaransa ilipoteza wanajeshi wake 13 katika ajali kati ya helikopta mbili zilizokuwa katikaoperesheni nchini Mali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.