Pata taarifa kuu
ANGOLA-MAUAJI-USALAMA

Angola: Vikosi vya usalama vyashtumiwa kuhusika na mauaji

Shirika la kimataifa la haki za binadamu la Amnesty International na Omunga, shirika la haki za binadamu nchini Angola, yanashtumu vikosi vya usalama nchini humo kwa kuhusika na mauaji ya watu 7 katika kutekeleza sheria za kupambana dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 tangu kuzuka kwa ugonjwa huo mwezi Mei.

Luanda, Juni 8, 2020. Afisa wa polisi akitoa ulinzi katika mtaa mmoja huko Hoji-Ya-Luanda wakati watu wakiandamana dhidi ya ukosefu wa chakula wakati wa masharti ya raia kutotembea yakiendelea.
Luanda, Juni 8, 2020. Afisa wa polisi akitoa ulinzi katika mtaa mmoja huko Hoji-Ya-Luanda wakati watu wakiandamana dhidi ya ukosefu wa chakula wakati wa masharti ya raia kutotembea yakiendelea. OSVALDO SILVA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Watu hao, ambapo mwenye umri mdogo alikuwa na miaka 14, waliuawa kwa kukiuka hali ya dharura.

Kulingana na uchunguzi uliochapishwa Jumatatu (Agosti 24) na mashirika haya, polisi na jeshi wanatekeleza vitendo vya kikatili kwa kisingizio cha kuheshimisha hatua zilizowekwa katika kudhibiti kusambaa kwa virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa wa Covid-19.

Tumeona jeshi na polisi vikitumia nguvu za kupita kiasi na wakati mwengine kufanya ukatili katika kutekeleza masharti yaliyowekwa katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 nchini Angola. Hii ilisababisha mauaji ya vijana kadhaa. Polisi na jeshi nchini Angola hawasiti kutumia silaha zao kwa kutekeleza machafuko hayo kwa kisingizio cha kuheshimosha hatua zilizowekwa dhidi ya ugonjwa wa Covid-19, yamesema mashrika hayo katika taarifa ya pamoja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.