Pata taarifa kuu
CONGO-LISSOUBA-SIASA

Congo-Brazzaville: Rais wa zamani Pascal Lissouba aaga dunia Ufaransa

Pascal Lissouba amefariki dunia mapema Jumatatu asubuhi Agosti 24 huko Perpignan, Kusini mwa Ufaransa, familia ya rais wa zamani wa Congo imesema.

Pascal Lissouba, rais wa zamani wa Congo-Brazzaville.
Pascal Lissouba, rais wa zamani wa Congo-Brazzaville. Issouf SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mkewe, Jocelyne, na mwanae ambaye ni mbunge, Jérémie Lissouba walikuwa karibu naye kabla ya kufariki kwake. Alikuwa na umri wa miaka 88.

Pascal Lissouba ambaye alichaguliwa kidemokrasia mwaka 1992 na kupinduliwa mwezi Oktoba 1997 na Denis Sassou Nguesso wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Congo, alikuwa anaishi nchini Ufaransa baada ya kutoka uhamishoni jijini London, nchini Ungereza.

Katika miaka ya hivi karibuni, afya yake ilizorota. Alikuwa na ugonjwa wa Alzheimer na hakuweza tena kushiriki katika shughuli za kisiasa. alikuwa na muda mrefu haongozi tena chama cha UPADS, chama alichounda mwanzoni mwa miaka ya 1990 na ambacho kinaongozwa kwa sasa na Pascal Tsaty-Mabiala.

Ni rais wa pili wa Congo ambaye anafariki dunia nchini Ufaransa mwaka huu. Machi 30, Jacques Joachim Yhombi-Opango, aliyekuwa madarakani kati ya mwaka 1977 na 1979, alifariki dunia kutokana na ugonjwa wa Corona huko Neuilly-sur-Seine, katika mkoa wa Paris. Alikuwa na umri wa miaka 81.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.