Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-SIASA-USALAMA

Maandamano yapigwa marufuku Côte d'Ivoire hadi septemba 15

Serikali ya Côte d'Ivoire imepiga marufuku maandamano yoyote nchini humo hadi tarehe 15 Septemba, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Alhamisi baada ya makabiliano makali yaliyojitokeza hivi karibuni kabla ya kufanyika uchaguzi wa rais mwezi Oktoba.

Polisi wakiondoa vizuizi barabarani katika eneo la Yopougon, huko Abidjan  Agosti 13, 2020 baada ya maandamano. (Picha kumbukumbu)
Polisi wakiondoa vizuizi barabarani katika eneo la Yopougon, huko Abidjan Agosti 13, 2020 baada ya maandamano. (Picha kumbukumbu) SIA KAMBOU / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo inakuja wakati mashirika kadhaa ya kutetea masilahi ya wanawake nchini yamejiapiza kuandamana Ijumaa hii kupinga hatua ya rais Allassan Ouattara kuwania Muhula wa tatu.

Serikali ya Abidjan imetetea uamuzi wake huo kama njia ya kuzuia machafuko zaidi nchini.

Hivi karibuni rais wa Cote d’ Ivoire Alassane Ouattara, mwenye umri wa miaka 78, aliweka wazi msimamo wake kuwa atagombea kwa muhula wa tatu, hatua ambayo ilikuja baada ya kifo cha aliyekuwa waziri mkuu wake Amadou Gon Coulibaly Julai 8 ambaye alikuwa aliteuliwa kuwania kwenye nafasi hyo kwa tiketi ya chama tawala.

Miezi michache iliyopita, Rais wa Cote d'Ivoire alisema hatowania katika uchaguzi wa urais ujao na kuachia nafasi kwa kizazi kipya kuliendeleza taifa hilo la Afrika, lakini kifo cha Waziri Mkuu Amadou Gon Coulibaly ambaye alikuwa aliteuliwa kupeperusha bendera ya chama tawala katika uchaguzi wa urais, kilibadili hali ya mambo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.