Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA-MAUAJI

DRC: Watu 12 wauawa na askari huko Sange katika eneo la Ruzizi

Watu 12 wameuawa kwa risasi na askari ambao inadaiwa kuwa walikuwa katika hali ya ulevi. Tukio hilo lililotokea katika eneo la Sange, katika mkoa wa Kivu Kusini, Mashariki mwa DRC.

Askari wa FARDC katika mkoa wa Kivu Kaskazini.
Askari wa FARDC katika mkoa wa Kivu Kaskazini. AFP PHOTO/STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Hali ya wasiwasi imeripotiwa leo Ijumaa, Julai 31 huko Sange, katika eneo la Ruzizi, kilomita chache na mji wa Uvira. Askari mlevi wa FARDC alirusha risasi kadhaa, na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 12 ambao walifariki dunia papo hapo na wengine 9 kujeruhiwa.

Kulinagana na Radio ya Umoja wa Mataifa nchini DRC, Okapi, watu hao waliouawa ni wakazi wa kijiji cha Sange. Tukio hilo lilitokea usiku wa Alhamisi, Julai 30 majira ya saa mbili usiku katika vitongoji vya Kinanira na Rutanga, kilomita 33 Kaskazini mwa mji wa Uvira.

Kulingana na mkuu wa kijiji cha Sange, Ruhusu Malula, milio ya risasi ilikuwa bado inasikika leo Ijumaa asubuhi.

"Tangu mapema asubuhi ya leo, vijana wenye hasira wamekuwa wanakamata askari yoyote katika wanayekutana naye katika kijiji cha Sange." Kwa sasa barabara kuu namba 5 imefungwa katika maeneo kadhaa ili kuzuia magari" ,amesema mkuu wa kijiji cha Sange.

Waandamanaji wanaomba gavana wa mkoa wa Kivu Kusini kuzuru eneo la mashambulizi kabla ya mazishi ya ya watu hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.