Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-SIASA-USALAMA

Uchaguzi wa urais Cote d'Ivoire: Chama cha RHDP chakutana kumteua mgombea wake mpya

Wajumbe wa Chama tawala cha RHDP nchini Cote d'Ivoire wanakutana, ikiwa ni pamoja na rais wa nchi hiyo Alassane Ouattara kwa lengo la kumteua mjumbe wa chama hicho atakayepeperusha bendera ya chama katika uchaguzi wa urais wa mwezi Oktoba

Rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara wakati wa mkutano wa RHDP, Desemba 2019.
Rais wa Cote d'Ivoire Alassane Ouattara wakati wa mkutano wa RHDP, Desemba 2019. SIA KAMBOU / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wengi wana imani kuwa Alassane Ouattara atateuliwa kwenye nafasi hiyo.

Tangu kifo cha Waziri Mkuu Amadou Gon Coulibaly mapema mwezi Julai, wajumbe mbalimbali kutoka chama cha RHDP wamekuwa wakimshinikiza rais Ouattara kuwania katika uchaguzi wa urais wa mwezi Oktoba.

Wiki iliyopita, kwa ombi la mkurugenzi mtendaji wa chama tawala, Adamu Bictogo, wabunge na maseneta kutoka chama hicho, walikutana huko Abidjan, na kila mmoja aliomba rais Ouattara kuwania kwenye kiti cha urais katika uchaguzi wa urais.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Waziri wa Ulinzi na Kaimu Waziri Mkuu Hamed Bakayoko alitoa wito kwa rais Outtara kuwania kwenye kiti cha urais katika uchaguzi ujao.

Kinachosubiriwa kwa sasa ni uteuzi na kumsikia, mwenyewe rais Alassane Ouattara iwapo atakubali au la kuteuliwa kwenye nafasi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.