Pata taarifa kuu
MALI-ECOWAS-SIASA-USALAMA

Mali: ECOWAS yaomba wabunge 31 kujiuzulu

Viongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, wameendelea kujadili kuhusu hali inayojiri nchini Mali, katika mkutano wao wa kilele, ili kupata suluhisho la kudumu la mzozo wa Mali.

Rais wa Niger na Rais wa sasa wa ECOWAS, Mahamadou Issoufou, anawasili Bamako, Mali, Julai 23, 2020.
Rais wa Niger na Rais wa sasa wa ECOWAS, Mahamadou Issoufou, anawasili Bamako, Mali, Julai 23, 2020. MICHELE CATTANI / AFP
Matangazo ya kibiashara

ECOWAS imetishia kuchukuwa vikwazo kwa wale watakaopinga mpango wake wa kumaliza mzozo nchini Mali, na kuamua kuwa rais Ibrahim Boubacar Keïta ataendelea kusalia madarakani.

Hata hivyo upinzani umefutilia mbali maazimio ya jumuiya hiyo na kubaini kwamba wako tayari kuendelea na maandamano yao.

Utawala na upinzani bado wako kwenye vita vya wazi nchini Mali. Vuguvugu lilianzishwa Juni 5 (M5) pamoja na vyama vya upinzani na mashirika kadhaa ya kiraia wanaendelea kuombarais Ibrahim Boubacar Keïta ajiuzulu.

ECOWAS, katika mkutano huo ulioongozwa na rais wa Niger, Mahamadou Issoufou, ilichukua maamuzi muhimu. Kwanza, Jumuiya hiyo imeomba wabunge 31 waliochaguliwa na kupingwa na upinzani kujiuzulu, ikiwa ni pamoja na spika wa bunge Moussa Timbiné. Marais wa nchi za ECOWAS wamebaini kwamba hawatosita kuchukuwa vikwazo dhidi ya mtu yeyote atakayejaribu kuzuia mchakato wa amani.

Saa mbili za hotuba na mijadala na wakuu wa nchi hizo viliiwezesha ECOWAS kuchukuwa hatua kadhaa za vikwazo dhidi ya wale wote watakaochukua hatua kinyume na mchakato wa kuweka mambo sawa kwenye mgogoro wa Mali.

Katika mazungumzo yake na wenzake, Rais wa Mali Ibrahim boubacar Keitaanayeungwa mkono sana hakushindwa Keita ameyataja maandamano yaliyoandaliwa na Imam Dicko kuwa ni "jaribio la mapinduzi".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.