Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Miili 37 ya watu waliouawa yagunduliwa Pinga, Mashariki mwa DRC

Karibu miili 37 imegunduliwa hivi punde huko Pinga na viunga vyake, katika eneo la Walikale, katika mkoa wa Kivu Kaskazini, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Askari wa FARDC.
Askari wa FARDC. KUDRA MALIRO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo inasemekana kuwa idadi ya watu waliouawa inaweza kuongezeka kufuatia mapigano kati ya makundi mawili hasimu yaliyogawanyika kutoka kundi la waasi la Nduma Defense of Congo-Rénové (NDC-R).

Kwa muda wa siku mbili, mji wa Pinga umewekwa chini ya himaya ya vikosi vya jeshi la DRC (FARDC), lakini hali ni ya kutisha katika eneo ambalo mapigano hayo yaliripotiwa Ijumaa asubuhi Julai 24.

Kulingana na mwandishi wetu mjini Kinshasa, Patient Ligodi, ni vigumu kwa wakati huu kueleza idadi rasmi ya watu waliouawa au hasara zilizotokea katika mapigano ya Pinga na viunga vyake.

Vyanzo vya Monusco vimebaini kwamba miili ya watu wengi waliouawa iligunduliwa katika eneo hilo, ikiwa ni pamoja na ile ya wapiganaji kutoka makundi hayo mawili hasimu waliyogawanyika kutoka kundi la waasi la NDC-R, na raia wa kawaida. Angalau askari wanne wa FARDC ni miongoni mwa waathiriwa waliotambuliwa. Watu kadhaa wamejeruhiwa katika mapigano hayo.

Huko Pinga, hakuna kundi hata moja kati ya makundi hayo mawili lenye udhibiti wa mji huo ambao jeshi la FARDC linajaribu kuimarisha ngome zake.

Wakati huo huo wapiganaji 16 kutoka makundi hayo mawili walijisalimisha kwa askari wa India wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO. Walisafirishwa kwenda Goma na wanahudumiwa na mpango wa serikali wa kuwarejesha wapiganaji katika maisha ya kiraia.

Hata hivyo hali bado ni tete. Papigano pia yameripotiwa jana Ijumaa kati ya makundi hayo mawili katika mji wa Mutongo, kilomita 30 kutoka Pinga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.