Pata taarifa kuu
SOMALIA-USALAMA-SIASA

Bunge la Somalia lamtimua Waziri Mkuu Khayre

Bunge la Somalia limepiga kura leo Jumamosi ya kumwondoa kwenye wadhifa wake Waziri Mkuu Hassan Ali Khayre, ambaye ameendelea kusolewa kutokana na jinsi anavyoishughulikia hali ya usalama nchini humo.

Waziri Mkuu wa Somalia Hassan Ali Khayre ameachishwa kazi akishutumia kwa kutowajibika kushughulikia hali ya usalama.
Waziri Mkuu wa Somalia Hassan Ali Khayre ameachishwa kazi akishutumia kwa kutowajibika kushughulikia hali ya usalama. REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Wabunge wamepiga kura ya kumuachisha kazi Hassan Ali Khayre kwa kura 170 na wabunge wanane wamepiga kura ya hapana, ametangaza spika wa bunge la Somalia.

Rais wa Somalia Mohamed Abdullahi Mohamed amesema katika taarifa kwamba anakubali uamuzi wa bunge kumtimua waziri mkuu.

"Hivi karibuni atamteua waziri mkuu mpya," imesema sema taarifa hiyo

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.