Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

Rais wa DRC awataka wafuasi wa muungano wa chama tawala kuwa watulivu

Rais wa DRC Felix Tshisekedi ametoa wito wa utulivu katika muungano wa chama tawala, huku akisema hakuna mpango wa kuvunja muungano huo.

Rais wa DRC Félix Tshisékédi huko Bukavu, Oktoba 8, 2019.
Rais wa DRC Félix Tshisékédi huko Bukavu, Oktoba 8, 2019. Tchandrou Nitanga / AFP
Matangazo ya kibiashara

Matamshi ya Tshisekedi yamekuja wakati ambapo maandamano yamekuwa yakishuhudiwa nchini humo, kutokana na mvutano wa kisiasa ndani ya muungano huo kuhusu mageuzi ya Mahakama na uteuzi wa Mwenyekiti mpya wa Tume ya Uchaguzi.

Hata hivyo hatua ya Bunge la taifa nchini DRC kumteua Ronsard Malonda kuwa mwenyekiti wa Tume huru ya Uchaguzi (CENI) inaendelea kuzua mvutano nchini DRC.

Chama cha UDPS kinashtumu mshirika wake madarakani FCC kusababisha hali hiyo, kwa kwa kujivunia wingi wa viti katika Bunge.

Wiki iliyopita Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kupitia Waziri wa Mambo ya Ndani Gilbert Kankonde ilipiga marufuku maandamano yote yaliyotarajiwa kufa,nyika wiki hiyo kupinga uteuzi wa Ronsard Malonda kuwa mwenyekiti mpya wa Tume ya uchaguzi CENI nchini humo.

Hali hiyo inatokea wakati mvutano kati ya muungano wa CASH unaendelea kujitokeza baada ya hukumu ya kifungo cha miaka 20 dhidi ya Mkurugenzi kwenye ofisi ya rais Felix Tshisekedi, Vital Kamerhe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.