Pata taarifa kuu
GHANA-CORONA-AFYA

Coronavirus: Rais wa Ghana akanusha madai ya kupatiwa matibabu Uingereza

Rais wa Ghana Nana Akufo Addo amekanusha taarifa kuwa amekuwa akipata matibabu ya Corona nchini Uingereza, siku chache baada ya taarifa kwamba amejiweka karantini.

Rais Akufo-Addo alichukuwa uamuzi wa kujitenga kwa muda wa siku 14 kama hatua ya tahadhari inayoendana na protokali za kiafya za kukabiliana na ugonjwa huo hatari wa kuambukiza.
Rais Akufo-Addo alichukuwa uamuzi wa kujitenga kwa muda wa siku 14 kama hatua ya tahadhari inayoendana na protokali za kiafya za kukabiliana na ugonjwa huo hatari wa kuambukiza. Paul Marotta/Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumapili taarifa kutoka Ikulu, zilisema rais huyo alikuwa ameanza kujitenga kwa siku 14 baada ya mtu wa karibu naye kuthibitishwa kuambukizwa Corona.

Taarifa iliyotolewa na Waziri wa Habari wa Ghana, Kojo Oppong-Nkrumah ilithibitisha habari hizo na kufafanua kuwa, Rais Akufo-Addo alichukuwa uamuzi huo wa kujitenga kwa muda wa siku 14 kama hatua ya tahadhari inayoendana na protokali za kiafya za kukabiliana na ugonjwa huo hatari wa kuambukiza.

Hata hivyo taarifa hiyo ilisisitiza kuwa vipimo alivyofanyiwa rais Akufo-Addo vilionyesha kuwa hajaambukizwa virusi vya Corona na kwamba katika kipindi hiki cha karantini, atafanyia kazi zake za kiofisi katika Ikulu ya Jubilee.

Mwezi uliopita wa Juni, Rais Akufo-Addo alitangaza kuwa Waziri wa Afya wa nchi hiyo, Kwaku Agyeman Manu amepatwa na ugonjwa wa Covid-19.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.