Pata taarifa kuu
NIGER-MAUAJI-USALAMA

Wakulima 15 wauawa katika kijiji cha Yargamji, Nigeria

Watu waliojihami kwa silaha wamewauwa wakulima 15 Kaskazini Magharibi mwa Jimbo la Katsina, katika kile, polisi wametaja ni kisa cha wizi wa mifugo.

Afisa wa polisi akitoa ulinzi huko Daura, katika Jimbo la Katsina, Februari 2019.
Afisa wa polisi akitoa ulinzi huko Daura, katika Jimbo la Katsina, Februari 2019. PIUS UTOMI EKPEI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa polisi Gambo Isah ameliambia shirika la AFP kuwa watu wapatao 200 waliojihami kwa bunduki walishambulia  wakulima  hao kwenye kijiji cha Yargamji na kuua  watu 15, na kuwajeruhi wengine kadhaa.

Nigeria ni moja ya nchi za Afrika Magharibi ambazo zinaendelea kukumbwa zaidi na utovu wa usalama kutokana na makundi mbalimbali yenye silaha, hasa makundi ya wanamgambo wa Kiislamu wenye itikadi kali, ikiwa ni pamoja na kundi la Boko Haram.

Mapema mwezi Juni watu wasiopungua hamsini waliuawa katika mashambulizi mawili yaliyotokea katika vijiji viwili, Kaskazini Mashariki mwa Nigeria, mauaji ambayo yalidaiwa kutekelezwa na kundi la Islamic State Afrika Magharibi (ISWAP).

Mashahidi wanasema watu waliojihami kwa silaha za kivita wakiwa katika magari walikabiliana na kundi la wanamgambo linaloungwa mkono na serikali, lakini wanamgambo hao walizidiwa nguvu kutokana na idadi yao ndogo na hivyo kundi hasimu kutekeleza mauaji dhidi ya raia waliokuwa wakitoroka makazi yao, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.